Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Camara kuikosa Mbeya City, Stellenbosch watajwa

Muktasari:

  • Simba itavaana na Stellenbosch katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Aprili 20 na timu hizo zitarudiana Aprili 27.

Dar es Salaam. Katika kile kinachoonekana ni kumuandaa kipa wao Moussa Camara kwa ajili ya mechi za nusu fainali za Kombe la Shirikisho Afrika, Simba imepanga kutomtumia katika mechi ya Kombe la Shirikisho la CRDB, kesho Jumapili, Aprili 13, 2025 dhidi ya Mbeya City.

Mechi hiyo ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Mbeya City itachezwa katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam.

Katika mazoezi ya mwisho ambayo Simba imeyafanya leo mchana uwanjani hapo kujiandaa na mechi hiyo, Camara hakuwa miongoni makipa walioshiriki.

Makipa waliofanya program ya maandalizi ya mechi hiyo ni Aishi Manula, Ally Salim na Hussein Abel.

Camara alionekana akiwa amevaa mavazi ya kawaida na wakati wenzake wakifanya mazoezi yeye alikuwa amekaa nje ya uwanja katika mabenchi ya wachezaji wa akiba.

Kipa huyo Jumatano iliyopita aliibuka shujaa wa Simba baada ya kuokoa mikwaju miwili ya penalti ya Al Masry na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa penalti 4-1 zilizoifanya itinge hatua ya nusu fainali.

Licha ya ushindi wa mabao 2-0 katika dakika 90, mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ulilazimika kuamriwa kwa mikwaju ya penalti kwa vile Simba ilipoteza mechi ya ugenini kwa mabao 2-0.