Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern ya Harry Kane itatoboa?

UEFA Pict

Muktasari:

  • Shughuli ni pevu. Club Brugge itamaliza ubishi na Atalanta, huku AS Monaco ikitambua kasheshe linalowakabili mbele ya Benfica, wakati Celtic itaonyeshana kazi na Bayern Munich na wakali wa Uholanzi, Feyenoord wataulizana maswali na AC Milan ya Italia.

Na leo tena. Mechi za mchujo za Ligi ya Mabingwa Ulaya za kuwania tiketi ya kucheza kwenye mtoano wa hatua ya 16 bora zinapigwa usiku wa leo Jumatano, huku mashabiki wa mikikimikiki hiyo wakitambiana atakayezubaa, atapigwa.

Shughuli ni pevu. Club Brugge itamaliza ubishi na Atalanta, huku AS Monaco ikitambua kasheshe linalowakabili mbele ya Benfica, wakati Celtic itaonyeshana kazi na Bayern Munich na wakali wa Uholanzi, Feyenoord wataulizana maswali na AC Milan ya Italia. 

Hizi ni mechi za kwanza. Macho ya wengi yatakuwa kwenye mchezo wa Bayern kuona watafanya nini chini ya kocha Vincent Kompany.

Club Brugge na Atalanta ni mechi ya upinzani, ambapo Club Brugge mara ya mwisho kuifunga timu ya Italia Ulaya ilikuwa Oktoba 2003 na mechi 15 zilizofuatia imetoka sare sita na vichapo tisa. Monaco na Benfica ni utamu mwingine na takwimu zinaonyesha mara mbili timu hizo zilipokutana, sare moja na ushindi mara moja kwa Benfica.

Celtic itasaka ushindi wake wa kwanza mbele ya Bayern. Balaa ni zito.