Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcelona yamrejesha Rashford Man United

Muktasari:

  • Mshahara mkubwa wa Rashford pamoja na umri wake unaokaribia miaka 29, vinatajwa kuwa sababu zilizoifanya Barca kushindwa kumnunua moja kwa moja nyota huyo.

Barcelona, Hispania. Barcelona imeamua kutomsajili moja kwa moja mshambuliaji wa England, Marcus Rashford, na hivyo atarejea Manchester United baada ya kukataa kulipa ada ya Pauni 26 milioni (Sh91 bilioni) iliyohitajika kumnunua jumla nyota huyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya Hispania, Barcelona ilikuwa tayari kulipa nusu ya kiasi hicho pekee, sawa na Pauni 13 milioni (Sh46 bilioni), lakini Manchester United imekataa pendekezo hilo.

Rashford, mwenye umri wa miaka 28, amefanya vizuri akiwa Barcelona msimu uliopita baada ya kufunga mabao 14 na kutoa pasi 14 za mabao katika mechi 26 alizocheza, akichangia timu hiyo kutwaa ubingwa wa La Liga na Kombe la Hispania.

Hata hivyo, Barcelona imeamua kuelekeza nguvu zake kwa kumsajili Anthony Gordon kutoka Newcastle United kwa Pauni 70 milioni, (Sh246 bilioni) huku ikielezwa kuwa ubora wake na umri mdogo vilimpa nafasi kubwa zaidi kuliko Rashford.

Aidha, miamba hiyo ya Catalonia inaendelea na mipango ya kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa kumuwania Bernardo Silva wa Manchester City na Julian Alvarez wa Atletico Madrid, huku tayari ikiwa na nyota kama Lamine Yamal, Raphinha, Ferran Torres na Fermin Lopez.

Rashford alikuwa akipendelea kubaki Camp Nou, lakini sasa Manchester United ipo huru kusikiliza ofa kutoka klabu nyingine.

Arsenal, Tottenham Hotspur na Aston Villa zinatajwa kuwa miongoni mwa timu zinazomuhitaji, huku Real Madrid, Bayern Munich na Chelsea nazo zikihusishwa na nyota huyo.

Mshahara mkubwa wa Rashford wa Pauni 315,000 Sh1.11 bilioni) kwa wiki pamoja na umri wake unaokaribia miaka 29, zinatajwa kuwa sababu zilizoifanya Barca kushindwa kumnunua moja kwa moja nyota huyo.

Iwapo hatapata timu mpya kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu ujao baada ya Kombe la Dunia 2026, Rashford atalazimika kurejea Carrington kujiunga tena na Manchester United, licha ya kuonekana kutokuwa sehemu ya mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo.

Wakati huohuo, kipa Andre Onana, ambaye alikuwa kwa mkopo Trabzonspor na kuisaidia timu hiyo kutwaa Kombe la Uturuki, naye anakabiliwa na hatma isiyoeleweka Old Trafford baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Senne Lammens.

Manchester United inapendelea kumuuza Onana, lakini inaelezwa kuwa inaweza kushindwa kurejesha hata nusu ya Pauni 47.2 milioni (Sh166 bilioni) ilizolipa wakati ilipomsajili kutoka Inter Milan kutokana na kushuka kwa kiwango chake, umri wake kuongezeka na kukosekana kwa Klabu zilizo tayari kulipa ada kubwa kama hiyo kwa sasa.