Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba Gyokres amwaga machozi

Muktasari:

  • Gyokeres tayari ameshatangaza wazi kuwa hatarudi Sporting Lisbon. Video ya gari la kuhama iliyoonekana nje ya nyumba yake nchini Ureno ilisambaa sana mtandaoni.

London, England. Sakata la uhamisho wa mshambuliaji wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres, kwenda Arsenal linazidi kuchukua sura mpya kila na sasa hali hiyo inadaiwa kumuathiri sana baba wa staa huyo ambaye alimwaga machozi wiki iliyopita baada ya dili kushindwa kukamilika licha ya kila kitu kudaiwa kuwa sawa.

Gyokeres mwenye umri wa miaka 27, ndiye chaguo la kwanza kwa Arsenal katika nafasi ya mshambuliaji wa kati kwenye dirisha hili lakini mazungumzo juu ya dili lake yamekuwa na panda shuka nyingi.

Taarifa za hivi karibuni zinaeleza kuwa pande hizo mbili zimekubaliana kwa kauli tu juu ya ada ya uhamisho inayofikia Pauni 55 milioni , pamoja na nyongeza ya Pauni 8.6 milioni kama bonasi lakini bado kuna mkubwa umeibuka kuhusu muundo wa malipo hayo ya bonasi ambapo Sporting inahitaji bonasi hizo ziwe katika masharti rahisi.

Kiasi cha Pauni 8.6 milioni ambacho kitalipwa kama bonasi kawaida hulipwa kwa kuzingatia vipengele mbalimbali ikiwemo mchezaji kucheza idadi fulani ya mechi au kufunga idadi fulani ya mabao na Sporting inaona Arsenal imeweka masharti magumu kwenye hilo ikiwa pamoja na mchezaji atatakiwa kufunga mabao mengi ili kutolewa kwa bonasi hizo.

Kutokana na kukwama huko, Arsenal imekosa fursa ya kumsajili Gyokeres mapema ili aweze kushiriki katika ziara yao ya maandalizi ya msimu barani Asia jambo ambalo limeharibu mipango ya Mikel Arteta na kumuumiza sana baba wa staa huyu pamoja na familia yake kwa ujumla.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya A Bola, baba mzazi wa Gyokeres amefikia hatua ya kulia kutokana na namna Sporting Lisbon wanavyoshughulikia uhamisho wa mwanawe.

Klabu hiyo haijaonesha dalili yoyote ya kulegeza msimamo wao kuhusu madai ya kifedha, na sasa kuna hofu kwamba dili hilo linaweza kuvunjika kabisa.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa Arsenal haijafanya mawasiliano yoyote rasmi kwa siku sita mfululizo, hali inayoongeza wasiwasi kuwa huenda Gyokeres akakosa nafasi ya kutimiza ndoto yake ya kujiunga na klabu hiyo ya viunga vya Emirates.

Gyokeres tayari ameshatangaza wazi kuwa hatarudi Sporting Lisbon. Video ya gari la kuhama iliyoonekana nje ya nyumba yake nchini Ureno ilisambaa sana mtandaoni.

Wiki iliyopita alikataa kurudi mazoezini na hakuwepo katika kikosi cha timu kilichoondoka kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu mpya.

Rais wa Sporting Lisbon, Frederico Varandas, ameendelea kuwa na msimamo mkali kuhusu suala hilo akisema:"Kama hawataki kulipa thamani halisi ya Viktor, tuko vizuri kabisa naye kwa miaka mitatu ijayo.

Hakuna aliye juu ya maslahi ya klabu. Tuko watulivu. Kila kitu kitaamuliwa kabla ya soko kufungwa, kwa faini kubwa na kuomba msamaha kwenye kikosi."