Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz Ki kukipiga AFCON mwakani, aitwa timu ya Taifa Burkina Faso

Nyota wa Yanga, Stephane Aziz Ki, amepenya katika mchujo wa mwisho wa kocha Hubert Velud na sasa atakuwa miongoni mwa nyota 27 watakaoiwakilisha Burkina Faso katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani huko Ivory Coast.

Kiwango bora ambacho amekionyesha katika kikosi cha Yanga msimu huu akikifungia mabao 10 na kupiga pasi mbili za mwisho kwenye Ligi Kuu pamoja na kucheza mechi zote za Ligi ya Mabingwa Afrika kinaonekana kumkosha Velud ambaye ameamua kwenda naye Ivory Coast baada ya kuwapungua wachezaji 28 kutoka kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 55.

Kikosi cha mwisho cha Burkina Faso ambacho Aziz Ki amejumuishwa, kitategemea zaidi safu ya ulinzi inayoongozwa na beki aliye katika kiwango bora kwa sasa wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani, Edmund Tapsoba.

Kocha Velud amejaza idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa katika Ligi Kuu mbalimbali Ulaya wakiwemo watatu wanaocheza katika Ligi Kuu ya England, Bertrand Traore (Aston Villa), Issa Kabore (Luton) na Dango Ouattara (Bournemuth).

Makipa wanne wameitwa katika kikosi cha Burkina Faso kitakachoshiriki AFCON ambao ni Herve Koffi, Hillel Konate, Kilian Nikiema na Sebastien Tou.
Mabeki waliopenya ni Issa Kabore, Steeve Yago, Issoufou Dayo, Nasser Djiga, Edmond Tapsoba, Abdoul Guiebre na Valentin Nouma.

Viungo ni Blati Toure, Adama Guira, Dramane Salou, Ismaila Ouedraogo, Sacha Banse, Gustavo Sangare na Azik Ki.
 Kundi la washambuliaji lina Bertrand Traore, Dango Ouattara, Hassane Bande, Mohamed Konate, Fessal Tapsoba na Cedric Badolo.