Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz Ki atupia manne Yanga ikiinyeshea Stand United

Muktasari:

  • Aziz Ki ambaye ameibuka mchezaji bora wa mchezo huo amefunga mabao manne na kutoa pasi mbili za mabao.

Dar es Salaam. Yanga imepata ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya Stand United katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB uliochezwa kwenye uwanja wa KMC, Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo nyota wa Yanga, Stephen Azizi Ki amepachika mabao manne ambayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kipigo hicho cha fedhea kwa Stand United.

Azizi Ki ndiyo alikuwa wa kwanza kuingia kambani katika dakika ya 16 akitumia vyema pasi ya Kibwana Shomari kabla ya Nickson Kibabage kufunga bao la pili katika dakika ya 20 na Clatous Chama ambaye amefunga mawili katika dakika ya 32 na 41.

Dakika ya 55 Azizi Ki alirudi tena kambani akifunga bao kupitia mpira wa adhabu baada ya Jonathan Ikangalombo kuchezewa vibaya karibu na eneo la hatari huku bao la tatu akifunga katika dakika ya 58 kabla ya kufunga lingine la nne dakika ya 66 huku bao la nane likiwekwa kambani na Kennedy Musonda.

Mbali na kufunga mabao manne Azizi Ki ameonyesha kiwango bora kwani amechangia kupatikana kwa mabao mengine mawili baada ya kutoa pasi mbili za mwisho kwa Nickson Kibabage, na Clatous Chama.

Hadi dakika 90 zinamalizika, Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho la CRDB, Yanga wameendelea kuonyesha kwamba bado wana hamu ya kulitetea taji lao baada ya kutoa kipigo hicho dhidi ya Stand United ambayo bao lake la kufutia machozi lilifungwa na Msenda Senga katika dakika ya 49.

Baada ya matokeo hayo, Yanga imetinga katika hatua ya nusu fainali na itacheza dhidi ya JKT Tanzania ambayo ilishinda mchezo wa jana mabao 3-1 dhidi ya Pamba Jiji.

Mchezo unaofuata Yanga itasafiri kwenda Babati, mkoani Manyara kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa kucheza dhidi ya Fountain Gate katika mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambako napo imekuwa ikifanya vizuri kwani hadi sasa inaongoza Ligi ikiwa na pointi 67 katika michezo 25.