Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz Ki aachana na Wydad, atua Al Ittihad

Muktasari:

  • Stephane Aziz Ki alijiunga na Wydad AC, Mei mwaka jana na akawa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichocheza Kombe la Dunia la Klabu.

Dar es Salaam. Kiungo Stephane Aziz Ki ameachana na Wydad AC ya Morocco na kujiunga na Al Ittihad ya Libya kwa mkataba wa miaka miwili.

Aziz Ki ambaye alijiunga na Wydad, Mei mwaka jana, ameachana na Wydad baada ya kuitumikia timu hiyo kwa muda wa miezi nane tu tangu alipojiunga nayo kutokea Yanga.

Usajili wa nyota wa zamani wa Sevilla na timu ya Taifa ya Ufaransa, Wissam Ben Yedder ambao Wydad itaukamilisha hivi karibuni, unaonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa kuishawishi klabu hiyo kumfungulia mlango wa kutokea Aziz Ki.

Inaripotiwa kuwa Al Ittihad imelazimika kulipa kitita cha Dola 300,000 ili kuipata saini ya kiungo huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Burkina Faso.

Al Ittihad imeonekana kuzizidi kete, MC Alger na Kaizer Chiefs ambazo pia zilikuwa zikimuwania kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 29.

Ndani ya kikosi cha Wydad AC, Aziz Ki amekuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa wakipata nafasi ya kutosha ya kucheza tangu msimu huu ulipoanza.

Mchezaji huyo hadi sasa ameichezea Wydad AC idadi ya mechi 11 ambapo kati ya hizo, saba alianza katika kikosi cha kwanza na nne aliingia kutokea benchi.

Katika mechi hizo 11 alizoichezea Wydad ambazo saba ni za Ligi Kuu ya Morocco na nne za Kombe la Shirikisho Afrika, Aziz Ki amefumania nyavu mara mbili huku akiwa hajawahi kupiga pasi ya mwisho.

Wydad ilivutika kumsajili Stephane Aziz Ki baada ya kukoshwa na kiwango bora alichoonyesha katika kikosi cha Yanga msimu wa 2023/2024.

Katika msimu huo, Aziz Ki alimaliza akiwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupachika mabao 21.

Mbali na kuwa Mfungaji Bora, Aziz Ki pia aliibuka mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huo.