Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kuvaana na PSG usiku wa Ulaya

Muktasari:

  • Mchezo wa nusu fainali ya pili utafanyika kwenye dimba la Parc des Princes, Mei 7 mwaka huu na mshindi wa jumla atafuzu kucheza fainali na mshindi kati ya Barcelona au Inter Milan ambazo zitakutana kesho.

Arsenal itaikaribisha PSG leo Aprili 29, 2025 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaochezwa kwenye uwanja wa Emirates saa 4:00 usiku kwa muda wa Tanzania.

Arsenal ilitinga katika hatua ya nusu fainali baada ya kuwaondoa mabingwa watetezi wa mashindano hayo Real Madrid ambapo ilipata ushindi wa jumla wa mabao 5-1, ikishinda mabao 3-1 nyumbani na kushinda mabao 2-1 ugenini.

PSG ilifuzu kucheza katika hatua ya nusu fainali baada ya kuiondoa Aston Villa kwa jumla ya mabao 5-4 ikishinda mabao 3-1 katika mechi ya kwanza na mchezo wa marudiano ilipoteza kwa mabao 3-2.

PSG ambayo tayari imeshatwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama 'Ligue One' imekuwa na wakati mzuri katika Ligi hiyo ikikusanya pointi 78 katika mechi 31.

Arsenal na PSG zilikutana Oktoba, Mosi mwaka jana katika mchezo wa hatua ya Ligi ya UEFA uliochezwa kwenye uwanja wa Emirates huku Arsenal ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyowekwa wavuni na Kai Havertz pamoja na Bukayo Saka.

PSG inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu ya kuiondoa Liverpool katika hatua ya 16 bora kwa mikwaju ya penati 4-5 baada ya kila timu kupata ushindi wa bao moja kwenye michezo yao ya ugenini.

Katika hatua ya 16 bora Arsenal ilifuzu kibabe kwenda robo fainali baada ya kuiangushia kipigo kizito PSV Eindhoven kwa kuifunga jumla ya mabao 9-3 ambapo mchezo wa kwanza Arsenal ilishinda mabao 7-1 ugenini na kupata sare ya mabao 2-2 nyumbani.

Thomas Partey hatakuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kitakachoivaa PSG kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano. Jorginho ambaye amekuwa mbadara wa kiungo huyo naye atakuwa nje ya kikosi akiwa bado ajawa fiti baada ya kutoka kuuguza majeraha.

Mchezo wa nusu fainali ya pili utafanyika kwenye dimba la Parc des Princes, Mei 7 mwaka huu na mshindi wa jumla atafuzu kucheza fainali na mshindi kati ya Barcelona au Inter Milan ambazo zitakutana kesho.