Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arajiga apewa tena Kariakoo Dabi

Mwamuzi Ahmed Arajiga

Muktasari:

  • Yanga imepata ushindi katika mechi tano mfululizo za mashindano zilizopita ambazo ilikutana na Simba.

Dar esSalaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemtangaza mwamuzi Ahmed Arajiga, kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii utakao wakutanisha Yanga dhidi ya Simba.

Ofisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo, amesema Arajiga atakuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo huo, akisaidiwa na Mohammed Mkono, atakayekuwa mwamuzi msaidizi wa kwanza na Kassim Mpanga, atakayekuwa mwamuzi namba msaidizi namba mbili.

Aidha Ndimbo amesema, mwamuzi wa nne atakuwa Ramadhan Kayoko kwenye mchezo huo ambao utapigwa kesho Uwanja Benjamin Mkapa

Rekodi zinaonyesha hii itakuwa ni Dabi ya tano kwa mwamuzi huyo kutoka Babati kuamua mchezo huo.

Yanga ndio wenye bahati na Arajiga, ambapo kwenye mechi nne zilizoamuliwa na mwamuzi huyo, imeshinda tatu na kupoteza moja.

Arajiga anaipokea Dabi hiyo kutoka kwa wamuzi wa Misri, ambao walichezesha mchezo wa mwisho baina ya timu hizo, kwenye kufunga msimu uliopita wa Ligi, ambapo Simba ilichezea kipigo cha mabao 2-0.