Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Andrea Berta rasmi atua Arsenal

Muktasari:

  • Bosi huyo wa zamani wa Atletico Madrid, Berta ametua Emirates kuchukua mikoba ya Edu, aliyeachana na timu hiyo, Novemba mwaka jana.

LONDON, ENGLAND: Arsenal imethibitisha uteuzi wa mkurugenzi mpya wa michezo, Andrea Berta, ambaye kazi yake kubwa itakuwa kufanya usajili wa kuleta mastaa wapya kwenye kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta.

Bosi huyo wa zamani wa Atletico Madrid, Berta ametua Emirates kuchukua mikoba ya Edu, aliyeachana na timu hiyo, Novemba mwaka jana.

Mtaliano Berta, 53, atakabiliwa na shughuli pevu kwenye usajili wa dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi, ambapo kipaumbele cha Arsenal ni kunasa huduma ya straika mpya, ambapo kwenye orodha hiyo wamo supastaa wa RB Leipzig, Benjamin Sesko na fowadi wa mabao wa Newcastle United, Alexander Isak.

Berta amejipatia umaarufu mkubwa kwenye klabu ya Atletico baada ya kuwasajili wakali kama Rodri, Antoine Griezmann na Jan Oblak, ambao wamebadilika na kuwa mastaa wakubwa kabisa wakiipa timu hiyo faida ya maana.

Berta alitangaza kuondoka Atletico mwanzoni mwa msimu huu baada ya kutumikia timu hiyo kwa miaka 12. Katika kipindi chake alichokuwa na Atletico, Berta alifanya mambo makubwa sana kumsaidia kocha Diego Simeone kushinda La Liga mara mbili, UEFA Super Cup na Europa League.

Na sasa atahamishia makali yake ya usajili kwenye kikosi cha Arsenal chini ya kocha Arteta. Wakurugenzi wa michezo mingine waliokuwa wakihusishwa na kibarua hicho cha kwanza kurithi mikoba ya Edu walikuwa Dan Ashworth, Roberto Olabe wa Real Sociedad na Thiago Scuro wa AS Monaco.

Mkurugenzi wa michezo wa kipindi cha mpito kwenye kikosi cha Arsenal, Jason Ayto, naye alitajwa kama anaweza kushikilia kiti hicho, lakini sasa mikoba amepewa Berta, ambaye sasa atashughulika na mambo ya usajili.

“Nimevutiwa na kitendo cha kujiunga na Arsenal katika kipindi kizuri kabisa klabuni,” alisema Berta.

“Nimeona kwa jinsi Arsenal inavyofanya mambo yake kwa miaka ya hivi karibuni na nimevutiwa na mpango wa kurudisha timu hiyo kwenda kuwa tishio kubwa Ulaya na duniani.”