Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alonso aongoza mbio kuinoa Chelsea

Muktasari:

  • Mbali na Alonso majina mengine yanayotajwa ni nyota wa zamani wa Chelsea, Cesc Fàbregas na Filipe Luís.

London, England. Klabu ya Chelsea imeanza kufanya mazungumzo ya chini kwa chini kwa ajili ya kumnasa Meneja wa zamani wa Real Madrid na Bayer Leverkusen, Xabi Alonso, kuwa Meneja mpya wa timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Alonso ambaye alifutwa kazi na Real Madrid mwezi Januari, miezi sita pekee tangu ajiunge akitokea Bayer Leverkusen, anaonekana kuwa chaguo la kwanza la mabosi wa Chelsea.

Kocha huyo Mhispania aliweka historia akiwa Leverkusen baada ya kutwaa ubingwa wa Bundesliga msimu wa 2023/24 bila kupoteza mchezo hata mmoja, lakini mambo hayakwenda sawa Madrid na sasa yupo huru kufanya mazungumzo na klabu yoyote.

Meneja wa Crystal Palace Oliver Glasner ambaye pia anatajwa kuwania nafasi ya kuinoa Chelsea. Picha na Mtandao

Mbali na Alonso, Chelsea pia imeweka majina mengine matano kwenye orodha ya makocha wanaowafuatilia akiwamo Andoni Iraola wa Bournemouth, Marco Silva wa Fulham na Oliver Glasner ambaye anatarajiwa kuondoka Crystal Palace mwishoni mwa msimu.

Majina mengine yanayotajwa ni nyota wa zamani wa Chelsea, Cesc Fàbregas na Filipe Luís.

Meneja wa Como, Cesc Fàbregas ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa Chelsea. Picha na Mtandao

Fàbregas ameendelea kung’ara akiwa Meneja wa Como 1907 inayoshiriki Ligi Kuu Italia ‘Seria A’ huku Filipe Luís akiwa amepata mafanikio na Flamengo baada ya kushinda Copa do Brasil kabla ya kuondoka mapema mwaka huu.

Taarifa zinaeleza kuwa Chelsea inataka kumpata kocha mpya ifikapo katikati ya Juni, huku uongozi wa klabu hiyo ukisisitiza unahitaji kocha wa muda mrefu mwenye uwezo wa kuendeleza vijana, kuendana na dira ya timu na kuleta matokeo ya ushindani.

Kwa upande wa Glasner, thamani yake imepanda baada ya mafanikio makubwa aliyoyapata Palace, ikiwamo kutwaa Kombe la FA msimu uliopita na Ngao ya Jamii, huku pia akiifikisha timu hiyo katika fainali ya Conference League.