Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alonso ang’atuka Madrid baada ya kichapo cha Barcelona

Muktasari:

  • Nafasi ya Alonso itakaimiwa na nyota wa zamani wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa ambaye anafundisha kikosi cha vijana cha klabu hiyo.

Real Madrid leo Jumatatu, Januari 12, 2026 imetangaza kuwa meneja wake Xabi Alonso amejiuzulu wadhifa wake kwa makubaliano binafsi.

Xabi Alonso ameondoka Real Madrid baada ya kuhudumu kwa zaidi ya miezi saba kama meneja.

Kiungo huyo wa zamani wa klabu hiyo ameondoka kwa makubaliano ya pande zote kufuatia kipigo cha mabao 3-2 ambacho imekipata kutoka kwa Barcelona katika fainali ya Kombe la Supercopa jana Jumapili, huku timu yake ikiwa nyuma kwa pointi nne dhidi ya klabu hiyo iliyo kileleni mwa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’.

Alonso alianza rasmi kazi Juni Mosi mwaka jana baada ya kipindi cha mafanikio akiwa Bayer Leverkusen, ambako alishinda mataji mawili ya ndani msimu wa 2023–24 na kuiongoza timu hadi fainali ya Ligi ya Europa.

Baada ya kuisimamia Real Madrid hadi nusu fainali ya Kombe la Dunia la Klabu, alianza kwa kuvutia kwa kushinda mechi 13 kati ya 14 zilizofuata, isipokuwa kipigo kikubwa cha dabi dhidi ya Atlético Madrid.

Kipigo dhidi ya Liverpool Novemba 4, 2025 kilianzisha mfululizo mbaya wa matokeo ulioshuhudia ushindi mara mbili tu katika mechi nane, na ingawa Alonso alijirekebisha kwa kushinda mechi tano mfululizo, maboresho hayo hayakuwa ya kutosha kuwashawishi viongozi wa klabu kwamba anapaswa kuendelea.

“Real Madrid inatangaza kuwa, kwa makubaliano ya pande zote kati ya klabu na Xabi Alonso, imeamuliwa kumalizwa kipindi chake kama kocha mkuu wa timu ya kwanza.

“Xabi Alonso ataendelea kuwa na mapenzi na heshima ya Mashabiki wote wa Madrid (Madridistas) kwa sababu yeye ni gwiji wa Real Madrid na amekuwa akiuwakilisha kwa uthabiti maadili ya klabu yetu.  “Real Madrid daima itakuwa nyumbani kwake.

Klabu yetu inapenda kumshukuru Xabi Alonso na benchi lake lote la ufundi kwa kazi yao kubwa na kujitolea katika kipindi hiki, na inawatakia kila la heri katika sura mpya ya maisha yao,” imefafanua taarifa ya Real Madrid.

Nafasi ya Alonso itakaimiwa na nyota wa zamani wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa ambaye anafundisha kikosi cha vijana cha klabu hiyo.