Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ahoua mtihani upo hapa kwa Simba

Muktasari:

  • Ahoua ambaye ni kinara wa mabao 12 katika Ligi Kuu kwa sasa  amecheza mechi 21, dakika 1457, kaanza mechi 17, katokea benchi michezo minne, ana asisti sita, mabao 12 kati ya hayo ya penalti ni  mabao matano.

Dar es Salaam. Kiungo mshambuliaji wa Simba, Jean Charles Ahoua je, anaweza akaifikia rekodi ya mabao 23 aliyoyafunga aliyekuwa straika wa timu hiyo Meddie Kagere ambaye kwa sasa anakipiga  Namungo FC inayonolewa na kocha Juma Mgunda.

Ni misimu saba imepita tangu rekodi hiyo iwekwe na Kagere ambaye alishindwa kuivunja hata yeye mwenyewe msimu uliofuatiwa wa 2019/20 aliyokuwa amemaliza na mabao 22.

Ahoua ambaye ni kinara wa mabao 12 katika Ligi Kuu kwa sasa  amecheza mechi 21, dakika 1457, kaanza mechi 17, katokea benchi michezo minne, ana asisti sita, mabao 12 kati ya hayo ya penalti ni  mabao matano.

Kutokana na data hizo Ahoua ana wastani wa kufunga bao moja katika mechi mbili, kwa michezo nane iliyosalia anaweza akafunga mabao manne, kitu ambacho  kinaonyesha ugumu wa kuifikia rekodi ya Kagere ambaye msimu huu katika timu anayoitumikia bado hajafungua akaunti ya mabao.

Kagere alicheza misimu minne Simba alifunga jumla ya mabao 65 ambapo 2018/19 mabao 23,  2019/20  mabao 22, 2020/21 mabao 13 na 2021/22 mabao 7.

Ingawa kocha wa Simba, Fadlu Davids anauamini uwezo wa washambuliaji wake akiwemo Ahoua kwamba watafunga mabao mengi, ila kuna wadau wengine wanaona kuivunja rekodi ya Kagere ya mabao 23 kwa mastraika wa wanaocheza Ligi Kuu ngumu, kutokana na mechi zilizosalia.

Straika wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein 'Mmachinga' ambaye aliandika rekodi ya mabao 26 mwaka 1999 inafikisha miaka 26, alisema haoni kwa msimu huu kama kuna mchezaji anaweza akafikisha mabao 23 ya Kagere.

"Kuna rekodi nyingi za mabao mfano ili mchezaji aifikie rekodi yangu atatakiwa aanze na ya Abdallah Juma aliyefunga mabao 25 aliyofunga mwaka 2006 ndipo zifuate nyingine," alisema.

Kwa upande wa Juma alisema:"Wachezaji wa sasa wakiamua kupambana wanaweza, kama Kagere aliweza hata wao inawezekana ingawa kwa msimu naona ngumu, kwa sababu zimesalia mechi chache, siyo Simba tu bali hata kwa washambuliaji wa Yanga."