Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Adaiwa kuua mke baada ya kunyimwa unyumba

Adaiwa kuua mke baada ya kunyimwa unyumba

Muktasari:

  • Fausta Silayo (22) Mkazi wa Kijiji cha Samanga wilayani  Rombo ameuawa kwa kuchomwa kisu na mume wake kwa madai ya kumnyima unyumba.

Rombo. Fausta Silayo (22), Mkazi wa Kijiji cha Samanga wilayani  Rombo ameuawa kwa kuchomwa kisu na mume wake kwa madai ya kumnyima unyumba.


Mwanamke huyo ambaye bado alikuwa uzazi wa mwezi mmoja alichomwa kisu Julai 23 na kupelekea kifo chake Julai 24 wakati alipokuwa amewahishwa Hospitali ya Huruma kwa ajili ya matibabu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwanamke huyo ambao amesema baada ya mwanaume huyo kufanya tukio hilo alikimbilia nchi jirani.


"Jeshi la polisi linaendelea na jitihada za kumtafuta mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye inasemekana amekimbilia nchi jirani ili kumkamata na kumchukulia hatua za kisheria,"amesema Kamanda Maigwa.


Kamanda Maigwa amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma ya Mkuu kwa maandalizi ya mazishi baada ya taratibu za uchunguzi kukamilika.