Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kajuna wa Simba afariki Dunia kuzikwa leo Kisutu

Klabu ya Simba imepata pigo baada ya mwanachama na kiongozi wake Idd Kajuna kufariki dunia baada ya kuugua kwa siku saba.

Kajuna amefariki leo Alhamisi, Julai 23, 2026 alfajiri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Hadi anafariki Kajuna alikuwa mjumbe wa kamati ya mashindano ya Simba, ambapo pia amewahi kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya timu hiyo.

Simba imethibitisha kifo hicho cha Kajuna huku ikitaarifu kuwa atazikwa leo katika Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

“Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa tarifa ya kifo cha aliyekuwa Makamu

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Iddi Kajuna kilichotokea usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Kajuna aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo mwaka jana na amehudumu kwenye nafasi hiyo hadi mauti yanamkuta huku kazi yake ya mwisho ikiwa ni Fainali ya Kombe la CRDB iliyofanyika Visiwani Pemba Julai 4 mwaka huu.

“Kajuna pia alikua Mjumbe wa Baraza la ushauri lilioundwa na Rais wa klabu Mohammed Dewji. Kabla ya hapo Kajuna amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba mwaka 2017 na Mjumbe wa kamati ya utendaji kuanzia mwaka 2014-2018.

“Kajuna pia amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya mpito ya Wakurugenzi mwaka 2018 wakati wa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa Uongozi,” imesema taarifa ya Simba.

Taarifa hiyo imesema kuwa mwili wa marehemu Kajuna utaswaliwa katika Msikiti wa Maamur Upanga na utazikwa katika Makaburi ya Kisutu Dar es Salaam leo Saa 10 Alasiri.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Crescentius Magori amesema Simba imepoteza mpambanaji jasiri wa klabu hiyo.

Magori amesema Kajuna hakuwa tu kiongozi bali alikuwa tayari wakati wote kuipigania Simba hata kabla ya kuteuliwa kwenye kamati hiyo.

"Hizi ni taarifa mbaya sana kwa Simba, tumepoteza mtu wa kupigana vitani, Kajuna ni msiba mkubwa ndani ya Simba. Alikuwa tayari wakati wote kuipambania Simba yake.

"Unaweza kusema labda uongozi lakini hapana alikuwa anaipigania klabu hii hata kabla ya kuwa kiongozi na hilo ndio likatufanya kumchagua kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano.

Taarifa zinasema Kajuna atazikwa eo jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.