Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sekta ya michezo ya kubahatisha inavyoigusa jamii ya Kitanzania

Michezo ya kubahatisha ni miongoni mwa sekta ambazo zimeshuhudia ukuaji mkubwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Ukuaji huu pamoja na mambo mengine umetokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta hiyo ambao umesababishwa na mazingira mazuri ya wawekezaji wengi kuamua kuwekeza nchini.

Uwekezaji huo unajumuisha kampuni mbalimbali za michezo hiyo kutoka ndani na nje ya Tanzania ambazo zimewekeza mitaji ya mabilioni ya fedha na kuwafanya wapenzi wa michezo hiyo wafurahie na uchumi wa nchi ukue.

Kwa mujibu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, sekta hiyo imechangia kiasi cha Sh 170 bilioni katika Pato la Taifa pamoja na kuzalisha ajira rasmi 25,000 ndani ya kipindi cha miaka 20 iliyopita.

SportPesa ikiwa ndiyo kampuni namba moja ya michezo ya kubashiri nchini ni miongoni mwa wawekezaji ambao wameleta manufaa makubwa katika Taifa hili.

Uwekezaji wa kampuni hiyo haujaishia katika michezo na burudani pekee bali umeenda mbali mpaka katika kuisaidia jamii ya kitanzania katika sekta mbalimbali.

Kuanzia afya, elimu mpaka mazingira SportPesa imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mkakati wake wa kurudisha kwa jamii.

Mfano Agosti mwaka huu, SportPesa wakiwa wadhamini wakuu wa Singida Fountain Gate FC walitembelea wodi ya wakina mama katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida ikiwa shamrashamra za kuelekea kilele cha maadhimisho ya “Singida Big Day” na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa.

Pia iliweza kukutana na baadhi ya wauguzi ikiwemo mganga mkuu wa hospitali hiyo na kusikia changamoto mbalimbali zinazokabili hospitali pamoja na mahitaji ya wagonjwa.

Jamii mbalimbali za kitanzania zimekuwa zikinuafaika na uwekezaji wa SportPesa ambao ndani ya kipindi cha miaka zaidi ya mitano ya uwekezaji wake nchini imegusa na kubadilisha maisha ya maelfu ya Watanzania.

Hakika umuhimu wa SportPesa haushii tu kwa kuwapa Watanzania burudani ya machaguo mengi ya michezo ya kubahatisha na kuwafanya wengine kuwa mamilionea, bali pia kugusa maisha ya wengine ambao sio wapenzi wa michezo hiyo.

SportPesa ni kampuni ya michezo ya kubahatisha ambayo inapendwa na watu wengi wa kubashiri pamoja na machaguo mengi yanayomuezesha mchezaji kuwa na nafasi kubwa ya kushinda fedha.