Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yamnyemelea Fermin López wa Barcelona

Muktasari:

  • Barcelona inatajwa kuhitaji fedha ili kuwasajili nyota wapya jambo linaloweza kuifanya ikubali kumwachia López licha ya mchango wake mkubwa.

London, England. Chelsea imeanza mazungumzo ya kumchukua kiungo wa Barcelona, Fermin López, huku ikitajwa kuwa tayari kulipa hadi paundi milioni 43 (Sh bilioni).

López, mwenye umri wa miaka 22, aling’ara msimu uliopita baada ya kucheza mechi 46, kufunga mabao manane na kutoa pasi 10 za mabao, akisaidia Barcelona kutwaa ubingwa wa La Liga.

Hata hivyo, msimu huu nafasi yake imeanza kutikisika kutokana na ushindani mkubwa wa viungo kama Pedri, Gavi, Frenkie de Jong na Dani Olmo.

Kwa upande wa Chelsea, dili hilo linaonekana kama sehemu ya mpango wa kuboresha kikosi kipya chini ya kocha Enzo Maresca, ambapo tayari wametumia zaidi ya paundi milioni 250 kwenye usajili wa wachezaji wapya wakiwemo João Pedro, Liam Delap na Jamie Gittens.

Barcelona inatajwa kuhitaji fedha ili kuwasajili rasmi nyota wapya akiwemo kipa Wojciech Szczesny, jambo linaloweza kuifanya ikubali kumwachia López licha ya mchango wake mkubwa.

Chelsea kwa upande wake imerudisha sehemu kubwa ya fedha ilizotumia kwa kuuza wachezaji kadhaa, akiwemo Carney Chukwuemeka (£24m, Dortmund), Noni Madueke (£52m, Arsenal) na João Félix (£26m, Al-Nassr).

Fermin López alizaliwa Mei 11, 2002 huko El Campillo, Hispania. Alijiunga na La Masia, akademi ya Barcelona, akiwa na umri mdogo kabla ya kukomaa kupitia timu za vijana.

Msimu wa 2022/23 ulikuwa wa mafanikio kwake baada ya kuibukia kwa mkopo Real Oviedo, alikocheza mechi 37 na kufunga mabao kadhaa yaliyompa umaarufu. Ndipo akarejea Barcelona na kupewa nafasi ya kudumu na Xavi Hernández.

Kiwango chake kilimfanya kuitwa timu ya taifa ya Hispania na alicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Andorra majira ya kiangazi mwaka jana. Pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa taji la Euro 2024, ingawa alicheza mechi moja pekee.

Kwa sasa López anatajwa kama kiungo mwenye kipaji cha kipekee kutokana na uwezo wake wa kushambulia, kukokota mpira na pia kupiga mashuti ya mbali.