Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'Bao' la Aziz Ki lavuruga waamuzi, wadau wacharuka

Muktasari:

  • Yanga ilikuwa inahitaji ushindi au sare ya mabao katika mechi dhidi ya Mamelodi Sundowns jana iweze kusonga mbele baada ya mechi ya kwanza hapa Dar es Salaam kumalizika kwa sare tasa.

Kumekuwa na maoni tofauti juu ya bao lililoonekana kuwa halali kwa Yanga katika mechi dhidi ya Mamelodi Sundowns jana huko Pretoria , Afrika Kusini likipachikwa na Stephane Aziz Ki katika dakika ya 57 huku wengi wakiamini kuwa lilistahili kukubaliwa na refa.

Mwamuzi Dahane Beida wa Mauritania aliyechezesha mechi hiyo kwa msaada wa waamuzi waliokuwa katika chumba cha teknolojia ya video ya usaidizi kwa marefa  (VAR) alikataa bao hilo ikitafsiriwa kuwa lilipaswa kukubaliwa kwa vile mpira mpira ulionekana ulivuka wote kwa asilimia mia moja.
                                              
"Watanzania wameporwa ushindi"-Gamondi

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa timu yake ilistahili kupata bao hilo ambalo lingeweza kuipeleka Nusu fainali huku akidai kuwa ulikuwa ni uporaji wa haki ya Watanzania.

"Sio jambo zuri kwa mpira wa Afrika kwa kile kilichotokea leo. Hii timu kubwa haiitaji msaada wa VAR. Nimesikitishwa na nadhani mashabiki wa Yanga wataona.(Marefa) Wamefanya uongo dhidi ya nchi," alisema Gamondi.


Mokwena apata kigugumizi

Kocha wa Mamelodi Sundowns, Rulani Mokwena alisema hawezi kujibu kama bao lililokataliwa la Yanga lilikuwa halali au sio halali.

"Sihitaji kujihusisha kwenye mjadala kama ni penalti au sio penalti. Kulikuwa na matukio mengine kama kiwiko na Divine Lunga ndani ya boksi ambayo ingeweza kuwa penalti. Hivyo siwezi kuzungumzia vitu hivyo labda kama ningepoteza ningeamua kuchukua uelekeo huo," alisema Mokwena.


Wadau wacharuka

Makamu wa zamani wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele alisema kuwa Yanga inapaswa kukata rufaa.
 
"Young Africans Sports Club inaweza kukata rufaa kwa chombo kinachoongoza mpira wa miguu (CAF) na rasmi waripoti upangaji wa matokeo chini ya ibara ya 16 kipengele cha 3 ambacho kinasema,Upangaji wa matokeo na makosa ya kiutawala kama yatahibitishwa, Mamelodi inaweza kuondolewa mashindanoni kwa faida ya Yanga.

Marefa tofauti nchini wametoa maoni yao juu ya bao ambalo Yanga ilikataliwa dhidi ya Mamelodi Sundowns jana katika mchezo wa marudiano wa haua ya robo fainali huko Afrika Kusini lililofungwa na Stephane Aziz Ki huku wakionekana kutofautiana.


Marefa wafunguka

Mwamuzi wa zamani nchini, Israel Nkongo alisema mwenye maamuzi ya mwisho kwenye mchezo ni mwamuzi hivyo hakuna sababu ya kutafuta mchawi.

"Huenda walikosea au walipatia kwa jinsi walivyoona wao ila mashabiki wanapaswa kutambua maamuzi ya mwisho yakishatolewa basi yanabaki kama yalivyo, katika maamuzi kuna watakaoumia na watakaofurahia hivyo tuheshimu yaliyotokea," alisema.

Erick Onoka ambaye pia ni mwamuzi mstaafu kutoka jijini Arusha alisema kilichotokea kwa upande wake anaona hakikuwa sawa kwa sababu Yanga ilistahili kupata bao hilo kutokana na mpira uliopigwa kuonekana wazi kupita mstari wa kati ya goli.

"Wengi wanahoji kwanini mwamuzi hakwenda kuangalia mwenyewe tukio lile lakini ninachokifahamu endapo kutakuwa na utata ndipo wale wasaidizi wake kwenye vyumba wanaweza kumuita akajiridhishe, kwangu Yanga imenyimwa bao halili kabisa."

Kwa upande wa mwamuzi mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini alisema, ameshangazwa na maamuzi yaliyofanyika kwani ni dhulma ya wazi iliyofanyika kwa kuikosesha timu hiyo nafasi ya wazi ya kusonga nusu fainali ya mashindano hayo.

Katika mchezo huo, Mamelodi Sundowns iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 za mchezo zikiwa hazijafungana.


Mitandao yachafuka

Mashabiki wengi wa soka hasa Afrika Kusini wameonyeshwa kuduwazwa na uamuzi uliochukuliwa na refa wa kukataa bao hilo na wametumia kurasa za mutandao yao ya kijamii kupaza sauti zao.