Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nakupenda Mama

Mama na mwana

Muktasari:

Mvua baridi na jua, nguo ulinifunika,

Nilipoanza kulia,  na nyimbo zilikutoka,

Mema ulonipatia, jamii yanufaika,

Mama nakupenda sana, mama hakuna mwingine

Zawadi gani nikupe, mama uliyenizaa,

Moyo ukae mweupe, furaha ikakujaa,

Deni wapi nikalipe, ni zamu ya kukulea,

Tuseme basi Amina, iwe heshima kwa mama.

 

Ulilala kwa kilepe, pale nilipougua

Ulisaka kama kupe, mwanao nisife njaa,

Nikisema nikulipe nitamaliza dunia,

Tuseme basi Amina, iwe heshima kwa mama.

 

Mvua baridi na jua, nguo ulinifunika,

Nilipoanza kulia,  na nyimbo zilikutoka,

Mema ulonipatia, jamii yanufaika,

Mama nakupenda sana, mama hakuna mwingine.

 

Nakupenda sana mama, kweli hakuna mwingine,

Mama  usishike tama, machozi yasinidone,

Na Mungu akupe mema, mabaya yasikuone,

Mama nakupenda sana, mama hakuna mwingine.

 

Usemi ningerudia, hivi nani kama mama

Elimu ulonipatia, hakuna dunia nzima,

Huzuni itanijia, tekelea ikihama,

Useme basi Amina, iwe heshima kwa mama.

 

Asante kwa yote mama, mwishoni najisemea,

Dua zako kwa labama, upate kuniombea,

Hakuna wa kukupima, Mlojo sijakosea

Mama nakupenda sana, mama hakuna mwingine.

Mashairi ya Mlojo- 0717 422233,  0179 571076