Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moyes kutoka mteule hadi mkosefu Manchester Utd

David Moyes

Muktasari:

Hii ni mara ya kwanza tangu Novemba 6 1986, Manchester United wanamtimua kocha wake.

 

London, England. Hatimaye Manchester United imemtimua kocha wake  David Moyes ikiwa ni miezi 10 baada ya kuteuliwa kuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson.

Moyes ametimuliwa baada ya mkutano mrefu na Mkurungenzi Mtendaji wa Man United, Ed Woodward kwenye uwanja wa mazoezi  Carrington.

Moyes (50) alipendekezwa na Ferguson kuwa mrithi wake wakati alipostaafu baada ya kuifundisha timu hiyo kwa miaka 26 msimu uliopita.  Kwa mujibu wa BBC,  kocha Steve Round na Jimmy Lumsden ameondoka pamoja na bosi wao.

Awali klabu hiyo ilikataa kuzungumza na BBC gazeti hilo la serikali kuhusu taarifa za kutimuliwa kwa Moyes Jumatatu iliyopita. Moyes aliondoka Everton na kusaini mkataba wa miaka sita na vigogo hao wa Ligi Kuu England, lakini amefukuzwa kabla ya  kumalizika kwa msimu huu.

Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa jana ilisema:  “Napenda kutumia nafasi hii kumshukuru kwa kazi ngumu aliyoifanya, ukweli na kujitoa kwake alikoonyesha hapa.”

Mtandao wa Sportsmail umebaini kuwa beki wa zamani aliyekuwa katika benchi la ufundi chini ya Moyes, Phil Neville, amebaki klabuni hapo.

Man United, ambayo kwa sasa ipo nafasi ya saba katika msimamo ikiwa imepoteza ubingwa wake licha ya kusaliwa na michezo minne, imejiweka  katika mazingira ya kumaliza msimu ikiwa katika nafasi mbaya zaidi kuliko wakati mwingine katika kipindi cha zaidi bya miaka 20.

Wakiwa chini ya Moyes wamepoteza mechi sita za ligi wakiwa nyumbani, walitolewa katika Kombe la FA na Swansea wakifungwa kwenye Uwanja Old Trafford na walishindwa kuwazuia Sunderland wasiwatoe katika nusu fainali ya Kombe la Ligi.

Machi baadhi ya mashabiki walikodi ndege na kupitisha bango la kutaka kocha huyo atimuliwe. bango hilo liliandikwa ‘Asiye Sahihi- Moyes aondoke’ (“Wrong One - Moyes Out”) wakijibu bango lililowekwa Old Trafford lililokuwa likimsifu Moyes kuwa ‘Mteule’ (“Chosen One”), wakati wa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Aston Villa.

Manchester United kwa mara ya kwanza watakosa Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu 1995. Pia kuna uwezekano wa kushindwa kufuzu kucheza Europa Ligi. Itakuwa ni mara ya kwanza kwao kukosa mashindano yote ya Ulaya tangu 1990. 

Man United walifanikiwa kufuzu kwa nane bora ya Ligi ya Mabingwa kabla ya kutolewa na Bayern Munich na Moyes alisifiwa kwa kuonyesha kiwango cha juu zaidi katika mashindano hayo.

Hata hivyo, Moyes amekuwa akishutumiwa kwa kukosa maelewano na baadhi ya wachezaji wake wa kikosi hicho.

Wakati kiungo Anderson alipojiunga kwa mkopo wa muda mrefu klabu ya Fiorentina mwezi Januari, alikaririwa akisema wachezaji wa United “wanataka kuondoka”,  japokuwa baadaye alikanusha.

Rio Ferdinand na Robin van Persie pia walitoa kauli za utata juu mfumo wa ufundishaji wa kocha huyo, huku Javier Hernandez na Wilfried Zaha wakitoa lawama zao katika twitter.

Moyes aliondoka Everton baada ya kukaa kwa miaka 11, akisema hawezi kukataa nafasi ya kuhamia Old Trafford na alianza kibarua chake Julai Mosi mwaka jana.

Hata hivyo, Man United walipata wakati mgumu katika usajili wake baada ya kushindwa kuwasajili nyota wawili wa Barcelona, Thiago Alcantara na Cesc Fabregas.

Moyes pia hakufurahishwa na United kupangiwa ratiba ngumu mwanzoni mwa msimu. Alipangwa kucheza na Chelsea, Liverpool na Manchester City katika mechi tano za mwanzo.  Lakini alianza vema msimu kwa kushinda 2-0 dhidi ya Wigan Athletic na kunyakua Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Wembley, akifutiwa na kupata ushindi 4-1 ugenini dhidi ya Swansea City.

Hata hivyo, mambo yalibadilika baada ya kufungwa na  Liverpool na Man City, na kuonyesha kwamba mwaka mbaya kwa Man United.

Moyes anakuwa kocha wa tatu kufundisha Man United kwa muda mfupi wengine ni Matt Busby (mechi 21) na Jimmy Murphy  (22)