Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TUONGEE KIUME: Mabinti wa kizazi hiki wanahitaji maombi

Binti mmoja aliandika kwenye mtandao wa kijamii akilalamika kwamba, kuna rafiki yake wa kiume, ni rafiki, siyo wapenzi, alimtafuta na kumuomba waende kutembea mbuga za wanyama wikiendi moja. Binti akakubali. Wakatoka Dar es Salaam, wakaenda mpaka mbugani. Huko wakachukua chumba kwenye hoteli ya kitalii ndani ya mbuga, chumba kimoja.

Mchana, binti na rafiki yake walikuwa wanakwenda kutembea, usiku wanalala pamoja na kufanya mapenzi. Hali ilikuwa hivyo kwa wikiendi nzima. Waliporudi Dar, rafiki alimrudisha binti mpaka nyumbani na kumpatia shilingi elfu thelathini… hapo kwenye elfu thelathini ndipo malalamiko ya binti yalipoanzia.

Binti analalamika kwamba, inakuwaje mtu aliweza kugharimia safari nzima kwa mamilioni ya pesa, kuanzia usafiri, hoteli, chakula, utalii na kadhalika, lakini akashindwa kumpa pesa ya kueleweka. Kisha akamalizia lawama zake kwa kusema, wanaume wa siku hizi hovyo kabisa.

Mrejesho alioupata sidhani kama ulimsaidia kwa sababu kila mtu, hususan wanaume walikuwa wanamuuliza, unafanyaje mapenzi na rafiki yako ambaye siyo mpenzi wako? Unakubali vipi kufanya mapenzi na rafiki yako wakati mlikwenda kutembea tu? Unafanyaje mapenzi na kutaka kulipwa? Je, unafanya biashara hiyo? Unatakaje kulipwa wakati mlikwenda kutembea? Je, mlikubaliana atakulipa? Ulitaka akupe shi ngapi na kwa nini?

Comment zilinichekesha na kunikumbusha moja ya mashairi kutoka kwenye kitabu cha Jinsi ya Kurudi Nyumbani cha Esther Mngodo. Shairi linaloongelea wanawake wanamuona mwanamke mwenzao barabarani akijiuza na kuanza kumuongelea vibaya na kumuita majina kwamba ni kahaba, ilhali wao wenyewe mtindo wao wa maisha unafanana kila kitu na kahaba kasoro tu wao hawasimami barabarani.

Na hiki ndicho kizazi cha sasa, ndio uhalisia. Sitaki kuwaita majina mabaya, lakini ukweli ni kwamba, madada wa mjini wa kizazi hiki wengi wanaishi kana kwamba wanafanya biashara. Tofauti yao ni kwamba, hawasimami barabarani.

Unakuta mwanamke mzuri anaishi kwenye nyumba ambayo inalipiwa kodi na wanaume zaidi ya wanne ambao sio ndugu zake. Hapa akichukua laki, pale laki na nusu, akichanganya ya kwa yule na ya huyu anakuwa na milioni moja na nusu analipa kodi ya miezi sita.

Simu kali anayotumia imenunuliwa kwa staili hiyo hiyo. Picha za dinner na mitoko anayopost kuumiza roho watesi wake yote alipelekwa pia. Leo anapelekwa na huyu, kesho na yule, analipaje? Sio uambiwe kila kitu, mtu mzima, jiongeze.

Narudia tena, sitaki kuwakosea heshima wanawake wa mjini wa kisasa, lakini kusema ukweli inabidi ifike mahali tukae na hawa mabinti zetu, dada zetu, tuwaambie ukweli tu; waache tabia ya kutamani kuwa na vitu wasivyoweza kuvimudu. Na kama wanashindwa kujizuia kuvitamani, basi hata waishie kwenye kuvitamani tu lakini sio kuvitaka. Wakishindwa kabisa, itabidi huu mwaka tufunge na kukiombea hiki kizazi.