Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuweka akiba ni tabia au uwezo wa kipato?

Kuweka akiba ya fedha kumeongezeka umaarufu katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na sababu kama ongezeko la gharama za maisha, maendeleo ya huduma za kifedha, elimu ya fedha, upatikanaji wa habari na mengine.

Hata hivyo, kwa mtazamo wa mazingira yetu, wengi wanaona kuweka akiba kuwa changamoto kutokana na hali duni ya kiuchumi. Wakati mwingine, inaonekana kuwa ni tabia inayowezekana kwa wenye vipato vikubwa pekee.

Swali ni: Je, kuweka akiba ya fedha ni uwezo wa kila mtu, au ni tabia inayoweza kupatikana hata kwa wenye kipato kidogo?

Ni hivi, uwekaji akiba una mizizi katika tamaduni za Kitanzania kupitia mazoea kama upatu na vikoba, ambapo wanachama huchangia fedha kwenye mfuko wa pamoja kwa manufaa ya baadaye.

Hii inaonyesha jinsi jamii ya Kitanzania inavyohifadhi pesa kama njia ya kinga wakati wa shida, kutokana na ufinyu wa vipato, kuweka akiba inakuwa jukumu la mtu mmoja, bali inafanikishwa kwa wajibu wa pamoja kwa mtindo wa kuchangiana.

Jambo hili linaakisi mambo mawili. Kwanza, wengi wanaoshiriki katika michezo hii mara nyingi wana kipato kidogo kisicho cha uhakika. Pili, licha ya hali hiyo, haikuzuia kuweka akiba; badala yake, imepelekea ubunifu katika mitindo ya uwekaji akiba, ikionyesha kwamba tabia ya kujiwekea akiba inatoa mwamko wa kutafuta suluhu bora ya uwekaji akiba, licha ya changamoto ya kipato.

Nadharia ya uchumi wa tabia “Mental Accounting” ya mwanazuoni Richard Thaler inatilia mkazo kwamba kuweka akiba ni mazoea ya kitabia ambapo mtu anaweza kuwa na akiba ikiwa atakuwa na tabia ya “kudunduliza” fedha pembeni katika kapu lake la akiba.

Thaler anasema watu huweka fedha zao katika makundi au malengo maalumu na wanakuwa na uwezo wa kufikia malengo hayo baada ya muda. Hii ina maana kwamba hata kama mtu ana kipato kikubwa, kama hana tabia ya kuweka akiba, hataweza kuwa na akiba ya fedha.

Hali hii inakubaliana na nadharia maarufu ya mwanauchumi Maynard Keynes, "Keynesian Psychological Law of Consumption," inayosema kwamba kadiri kipato kinavyoongezeka, mahitaji ya matumizi pia yanaongezeka. Usipokuwa na tabia ya kuweka akiba, hata ukiwa na pesa nyingi, ndio matumizi yatazidi zaidi.

Kwa upande mwingine, kuweka akiba ni jambo linaloathiriwa kwa kiasi kikubwa na uwezo wa kifedha. Watu wenye vipato vidogo visivyokuwa na uhakika, akiba zao kifedha hazikui, na wengi wanatumia pesa hizo katika mahitaji yao ya kila siku.

Takwimu za watumiaji huduma za kifedha nchini mwaka 2023 zinaonyesha kwamba takribani asilimia 77 ya Watanzania kipato chao fedha ni cha msimu, au kutokana na ajira za muda zisizotabirika, hiyo inaweza kukazia dhana hii kuwa, hata asilimia 47 ya Watanzania wanaoweka akiba, wanatumia akiba hizo kwa ajili ya mahitaji ya kila siku ya kujikimu, mfano chakula.

Katika tafsiri rahisi, ingawa kuweka akiba ya fedha ni tabia kama tulivyoona awali, lakini pia, uwezo wa kifedha au kipato ni muhimu na unachangia pakubwa katika kuamua tabia hiyo. Bila hivyo, uwekaji akiba kwa malengo ya kimaendeleo inakuwa ni ngumu, badala yake akiba ya fedha inakuwa kwa mahitaji ya kujikimu tu, ikiwa mtu kipato cha fedha ni kidogo.

Kwa kumalizia, kuweka akiba ya fedha inahitaji yote mawili, tabia na uwezo wa kipato. Ili kufanikisha hilo, kuna haja ya kupanua wigo wa huduma za kifedha, kukuza elimu ya kifedha kwa vikundi vya jamii kama Saccos, watu binafsi, na wengine, ili kujenga jamii ya Kitanzania yenye uelewa na ustawi mzuri wa kifedha na kiuchumi.