Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza aanza kazi, amtaja Trump

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Andy Burnham. Picha na Mtandao

London. Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Andy Burnham, ameahidi kuleta mabadiliko, ikiwamo kuimarisha uhusiano na Marekani na Ukraine, huku akitaja kuingia kwake madarakani kama “mhimili wa mabadiliko” utakaolisukuma taifa hilo mbele.

Burnham (56) leo Jumatatu, Julai 20, 2926 amechukua rasmi usukani wa taifa hilo baada ya kukutana na Mfalme Charles III katika Jumba la Buckingham, kutokana na kujiuzulu kwa mtangulizi wake, Keir Starmer.

Hatua hiyo inamfanya Burnham kuwa Waziri Mkuu wa saba wa Uingereza katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, akitokea Chama cha Labour kwa lengo la kurejesha utulivu wa kisiasa.


Hotuba ya kwanza ya Burnham

Akizungumza kwa mara ya kwanza nje ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa 10 Downing Street, Burnham amekiri kuwa imani ya wananchi kwa wanasiasa imeshuka kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi nchini humo.

Katika kuleta matumaini mapya, ameahidi mambo kadhaa katika utawala wake, ikiwamo kutangaza hatua za haraka za kutoa “nafasi ya kupumua” kwa kaya zinazokabiliwa na kupanda kwa gharama za maisha, pamoja na kuweka wazi vyanzo vya mapato vya kugharamia afua hizo.

Ametangaza kuwa agizo lake la kwanza akiingia ofisini ni kukomesha wimbi la watu wasio na makazi wanaolala barabarani, pamoja na kujenga nyumba nyingi zaidi za bei nafuu za halmashauri.

Pia, amesisitiza mpango wake wa kuondoa nguvu za kimaamuzi kutoka Mji Mkuu wa London (Westminster) na kuzipeleka katika mamlaka za mikoa na miji mingine ili kukuza uchumi wa viwanda.

Katika hotuba yake hiyo, Burnham ametangaza kuwa kabla ya mwisho wa mwaka huu ataweka hadharani mpango mkakati wa miaka 10 utakaoonesha mwelekeo mpya wa kiuchumi na kijamii wa Uingereza.


Mambo mazito yanayomsubiri

Burnham anaingia madarakani huku akikabiliwa na changamoto kubwa za ndani na nje ya nchi, ikiwamo masuala ya uchumi na kodi.

Tayari amepewa shinikizo kutoka kwa Kiongozi wa Chama cha Conservative, Kemi Badenoch, anayemtaka aruhusu upanuzi wa uchimbaji wa mafuta na gesi katika Bahari ya Kaskazini (North Sea) ili kukuza uchumi, hatua ambayo tayari imesifiwa na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Hata hivyo, Chama cha Green kimemtaka adhibiti bei za pango na kutaifisha sekta ya maji ili irudi mikononi mwa umma.


Uhusiano wa kimataifa

Burnham ameingia madarakani akiwa hana uzoefu mkubwa katika sera za kigeni, lakini ameshaweka wazi kuwa simu zake za kwanza zitakuwa kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, ili kuhakikisha msaada thabiti dhidi ya Urusi, pamoja na Rais Donald Trump wa Marekani kwa lengo la kujenga uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia.


Wasifu wa Burnham

Andy Burnham alizaliwa Januari 7, 1970  huko Lancashire, Kaskazini mwa Uingereza.

Alisoma katika shule za Serikali kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Cambridge, ambako alichukua Shahada ya Lugha ya Kiingereza.

Ni shabiki mkubwa wa soka, hususan klabu ya Everton FC, na anajulikana kwa tabia yake ya kujitofautisha na wanasiasa wasomi wa London kwa kuzungumza lugha rahisi inayoeleweka na wananchi wa kawaida.


Maisha ya siasa

Burnham alichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Leigh kwa mara ya kwanza mwaka 2001 na alidumu katika nafasi hiyo kwa miaka 16.

Alihudumu kama Waziri wa Utamaduni na baadaye Waziri wa Afya chini ya Serikali za Mawaziri Wakuu Tony Blair na Gordon Brown.

Baada ya kushindwa mara mbili katika kinyang’anyiro cha kuwania uongozi wa Chama cha Labour kitaifa dhidi ya Ed Miliband na Jeremy Corbyn, Burnham aliondoka bungeni mwaka 2017 na kugombea nafasi ya Umeya wa Jiji la Manchester.

Akiwa katika nafasi hiyo, alijizolea sifa kubwa kwa kupigania ugatuzi wa madaraka na haki za kiuchumi kwa maeneo ya kaskazini, jambo lililomfanya apewe jina la utani la “Mfalme wa Kaskazini”, hasa kutokana na kusimama kidete dhidi ya Serikali Kuu ya London wakati wa janga la Uviko-19.

Burnham alirejea bungeni hivi karibuni kupitia uchaguzi mdogo ulioratibiwa kimkakati na washirika wake, baada ya mtangulizi wake, Keir Starmer, kupoteza uungwaji mkono wa baadhi ya wabunge kufuatia wimbi la ukosoaji wa makosa ya kisiasa na mabadiliko ya maamuzi mara kwa mara.

Burnham alichukua uongozi wa chama bila kupingwa, na sasa amekuwa Waziri Mkuu rasmi bila kuhitaji mchakato mrefu wa uchaguzi wa ndani ya chama.


Imeandikwa na Noor Shija kwa msaada wa mtandao.