Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vyama 13 vya upinzani vyayapinga maandamano ya Chadema

New Content Item (22)
New Content Item (22)

Muktasari:

  • Muungano wa vyama 13 vya siasa umetoa tamko kuwataka Watanzania wasishiriki maandamano yaliyoandaliwa na Chadema Januari 24, 2024 vikisema yana dhamira ya kuvura amani

Dar es Salaam. Maandamano yaliyoitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo yameviibua vyama 13 vya  upinzani nchini na kutoa tamko la kuyapinga huku Chadema ikisema yapo palepale.

Vyama hivyo, vimewaomba Watanzania kutokushiriki maandamano hayo ya amani, vikidai yana dhamira ya kuvuruga amani ya nchi.

Maandamano hayo ya amani yalitangazwa Januari 13, 2024 na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikiwa ni maazimio ya kamati kuu ya chama hicho yamepangwa kufanyika Januari 24, 2024 kupinga miswada miswada mitatu iliyopo bungeni ya sheria za uchaguzi pamoja na ugumu wa maisha.

Leo Jumatano, Januari 17, 2024, viongozi wa vyama hivyo 13 wamekutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutoa msimamo wao huo.

Mwenyekiti wa umoja huo, Abdul Mluya amesema hata hoja zinazoelezwa na Chadema kama sababu ya kuandamana hazina msingi kwa hawakushiriki kutoa maoni kuhusu miswada hiyo ya sheria.

"Tunawaomba wananchi wasishiriki maandamano hayo na tunaomba Chadema itoke hadharani kuwaomba radhi kwa kwa hatua iliyochukuliwa ya kufanya maandamano “inakizana na utamaduni wetu," amesema Mluya.

Mluya ameendelea kuishtumu Chadema akidai kitendo chake wanakichukulia kama ubinafsi wa kutaka kusikilizwa wao wakati nchi ina mfumo wa vyama vingi vinavyotambuliwa kisheria.

“Serikali isiwaogope wao, ni chama kimoja lakini kinataka kupuuza mawazo ya wadau wengi waliotumia siku nyingi kutoa maoni katika kipindi ambacho wao waligoma kushiriki,” amesema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa ADC, Doyo Hassan amesema ni muhimu viongozi wa Chadema wakafikiria kutafuta mfumo sahihi wenye misingi ya kisheria kudai haki wanayotaka badala ya kufikiria maandamano.

“Kufanya maandamano ni hatua ya mwisho baada ya kujaribu mifumo mingine kushindikana, lakini watambue Wananchi wa kawaida ndiyo watapata madhara wakati wao na familia zao wakiwa wamejificha sehemu salama,” amesema.

Amesema muda wanaotumia kuhamasisha wananchi kufanya maandamano walitakiwa kutoa elimu kwa wananchi kufanya kazi kwa kutumia mvua zinazonyesha, ili wapate mavuno ya kutosha badala ya kuwataka kuingia barabarani.

Hoja iliyoungwa mkono na Katibu Mkuu wa UDP, Saum Rashid akisema uongozi si misuli bali ni hekima, busara na kuonyesha uwezo wa kutumia uzoefu na maarifa kuwaongoza wananchi.

“Ni muhimu kujenga kwanza na imani na vyombo vilivyopo katika kujenga misingi ya utawala bora kwa kujenga heshima za nchi yetu na kupata viongozi wanaowajibika, kwani madai wanayotaka kwa sasa hayawezi kupatikana kwa asilimia 100 kwa kuwa chama tawala kina wabunge wengi,” amesema.

Vyama vingine vinavyounda umoja huo ni pamoja na NRA, UDP, DP, ADC, Demokrasia Makini, TLP, SAU, CCK, AFP na Ada Tadea

Akizungumzia madai ya vyama hivyo,  Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema pamoja na tamko lao wao wanaweka pamba masikinioni, ratiba ya maandamano ibakia vilevile.

“Tunaweka pamba masikinioni, ratiba ya maandamano iko vilevile na Katibu Mkuu wetu ameshatoa ratiba ya namna shughuli zitakavyofanyika. Tunachokifanya sisi tunaratibu kwa niaba ya wananchi kwa kuwa Serikali haitaki kusikiliza maoni ya wadau na wanachokitaka,” amesema.

Akitangaza ratiba hiyo mapema leo, Katibu Mkuu John Mnyika amesema maandamano hayo ya amani yatakuwa na vituo viwili vikuuu yakianzia maeneo ya Mbezi karibu na stendi ya mabasi na mengine yakianzia Buguruni, na yote yatamalizikia ofisi za makao Umoja wa Mataifa (UN).