Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Sheikh Ponda atoa sababu kujiunga na ACT Wazalendo

Dar es Salaam. Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ametangaza kujiunga na chama cha ACT-Wazaendo akisema ameona umuhimu wa kuchangia nguvu katika operesheni ya ACT Wazalendo ya ‘Linda Demokrasia’, inayolenga kurejesha haki, uwazi na usawa katika michakato ya uchaguzi nchini Tanzania.

Amesema anajiunga na chama hicho lengo ni kuhakikisha: “Tunapata utawala wa sheria, na uchaguzi huru na wa haki.”

LIVE: Sheikh Ponda akitua ACT Wazalendo

Shekh Ponda ametangaza uamuzi huo leo Alhamisi Juni 5, 2025 makao makuu ya chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam na kupokelewa na viongozi waandamizi wa chama hicho wakiongozwa na kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu.

“Kwa muktadha huo natoa wito kwa vijana, wanawake, wazee, na viongozi wa dini kuungana katika uwanja wa mapambano ya kudai haki mbalimbali zikiwemo za kisiasa kama vile kuhakikisha kura zetu zinahesabiwa kwa haki, na viongozi wanaochaguliwa wanawakilisha matakwa ya wananchi,” amesema Sheikh Ponda.

Katibu wa Idara ya Itikadi, Mawasiliano kwa Umma wa ACT Wazalendo, Salim Biman (kulia) akimtambulisha kada mpya wa chama hicho, Sheikh Issa Ponda aliyepokewa katika makao makuu ya chama hicho Magomeni jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi Juni 5, 2025. Picha na Sunday George

“Ndugu zangu mnaonisikiliza, mapambano ya kudai haki si ya mtu mmoja wala chama kimoja bali yanahitaji umoja wa wapigania haki wote. Wale walioko katika vyama vya siasa, viongozi wa dini na kila Mtanzania anayejali mustakabali wa Taifa letu,” amesisitiza.


Endelea kutufuatilia Mwananchi