Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwalimu: Kuiacha CCM kupita bila kupingwa ni dhambi

Muktasari:

  • Kuiacha CCM kupita bila kupingwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba26, 2025 ni kosa dhambi kubwa katika kupigania mageuzi na demokrasia ya kweli.

Arusha. Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu amesema chama hicho kinatambua historia ya siasa za upinzani hazijawahi kuwa rahisi Afrika, lakini itakuwa dhambi kubwa kukiachia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupita bila kupingwa Uchaguzi Mkuu wa baadaye mwaka huu.

Akihutubia wananchi kwenye mwendelezo wa mikutano ya hadhara ya Chaumma For Change (C4C) uliofanyika Usa River jijini Arusha leo Alhamisi Juni 12, 2025. Mwalimu amesema kuna wanasiasa wa upinzani maarufu na wana ushawishi Afrika ikiwemo Raila Odinga nchini Kenya hajawahi kugomea uchaguzi.

Amesema njia pekee ya kuipindua Serikali iliyopo madarakani na kupata uhalali kutoka kwa wananchi ni kupitia sanduku la kura na si vinginevyo.

"Chaumma tumesema tunaenda kwenye uchaguzi tunaomba wananchi mtuunge mkono, tutaweka wagombea nchi nzima, Tunatambua historia ya vyama vya upinzani Tanzania na Afrika hazijawahi kuwa rahisi.

"Kuiacha CCM ishinde bila kupingwa ni dhambi kubwa katika kupigania mageuzi na uchumi wa kweli, tumesema tupo tayari kufia uwanjani," amesema Mwalimu.

Akifafanua hoja hiyo, Mwalimu amesema huko nyuma walitumia maarifa, nguvu, akili na fedha kuijenga taasisi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) itakayokuwa tayari kukabiliana na CCM.

"Tuliifanya kazi hiyo kwa bidii na uadilifu tukiamini Tanzania inahitaji mageuzi lakini safari hiyo ilianza kupigwa mawimbi na kujikwaa kwingi ndipo mihemko nayo ikaanza kuchukua nafasi.

"Tukaanza kusemana wenyewe na ujanja ukawa kuzodoana wenyewe, na ilifikia hatua mawimbi yaliongezekana na ujasiri tukaanza kutukanana, kufedheheshana tukafika mahala tukaanza kujadili uchaguzi tukitanguliza mihemko bila kuangalia mustakabali wa uhai wa taasisi," amesema Mwalimu.

Mwalimu katika maelezo yake amesema dhoruba hizo zilipoongezeka baadhi yao wakasema hapana ndipo waliamua kufungasha virago kwa amani kwenda kujiunga Chaumma.

"Tumekuwa tukipondwa na kuitwa majina mengi na adui wao sasa amekuwa Chaumma kila wanakopita wanaitukana na tunawauliza tatizo nini, wanashindwa kufahamu tulivyo sasa kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa ni kutofautiana kimawazo na mtizamo," amesema.

Amesema licha ya chama hicho kuendelea kusemwa, hakiwezi kurudi nyuma wanaenda kushiriki uchaguzi na wameanza kuwajengea ujasiri wananchi wakiamini safari ya mafanikio wakati wote si kujenga dhamira ya hofu.

"Unasemaje hauwezi kufanyika uchaguzi bila kufanya mabadiliko ya sheria, leo wanatubeza ipo siku watakuja kutupigia magoti na kuomba tufanye kazi pamoja, tuliona mbali muda ni mwalimu mzuri," amesema Mwalimu.

Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Chaumma Tanzania Bara, Devotha Minja amesema wametofautiana kimtazamo na Chadema, ni sababu ya wao kwenda kujiunga na Chaumma ili wakapambane na CCM.

"Huu si wakati wa kususa, huwezi kuisusia CCM, kama unaona nguvu zimeisha tafuta watu wengine waingie kwenye mapambano, Chaumma hata kama tutakuwa 10 tupo tayari kwenda kupambana hata kama wakituua wote tupo tayari," amesema.

Amesema chama hicho hakipo tayari kufunga ndoa na CCM, ndiyo maana wanahubiri sera yao ya ubwabwa kwa wote wakiingia madarakani wakatekeleze kwa ufasaha.

"Tupeni dola Chaumma tukahakikisha watu wote wanapata ubwabwa muda wote, tutajenga maghala ya chakula kwa wananchi, tupeni Chaumma nafasi tukaiondoe CCM ili wananchi wakapate furaha,"amesema Devotha