Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muasisi wa Chaumma ajiondoa, ataja sababu

Mmoja wa Wahasisi wa Chama Cha Chaumma,Eugene Kabendera akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, akitoa tamko la kujiondoa katika Chama hicho. Picha na Sunday George

Muktasari:

  • Eugene Kabendera kabla ya kujiondoa ndani ya chama hicho amewahi kuhudumu kama Naibu Katibu Mkuu wa Chaumma Tanzania Bara, mwakilishi wa Chaumma katika Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania na mgombea ubungo wa Ubungo mwaka 2015 na 2020.

Dar es Salaam. Mmoja wa waasisi wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Eugene Kabendera ametaja kujiondoa rasmi ndani ya chama hicho.

Kabendera ambaye pia amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chaumma Tanzania Bara, na mwakilishi wa Chaumma katika Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, ametangaza uamuzi huo leo Jumanne Mei 27, 2025.

Kupitia taarifa yake kwa umma, Kabendera ametaja sababu za kujiondoa katika chama hicho kuwa ni tofauti kubwa za kimtazamo kuhusu mwelekeo wa sasa wa Chaumma ambao kwa maoni yake hauendani tena na misingi ya kuanzishwa kwake.

“Huu ni uamuzi wa kimaadili unaotokana na msimamo wangu wa kudumisha uadilifu wa kisiasa na utumishi wa kweli kwa umma,” amesema Kabendera.

Bila kutaja mwendeleo wake baada ya uamuzi huo, Kabendera ambaye pia aligombea ubunge wa Ubungo mwaka 2015 na 2020, ameahidi kutoa ushirikiano kwa chama hicho pindi maono ya chama hicho yatakapoendana na maono yake.

“Nitaendelea kushiriki kikamilifu katika maisha ya kisiasa ya nchi yetu kwa uadilifu na dhamira ileile iliyoniongoza siku zote. Ninaondoka Chaumma nikiwa na moyo wa shukrani kwa wote tuliopambana pamoja kwa miaka hii 13.”

“Historia yetu haiwezi kufutika lakini ni wakati wa kuandika sura mpya kwa misingi ile ile ya haki, utu, na uadilifu,” amesema Kabendera.