Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamati Kuu Chaumma yajifungia kufanya uteuzi wa viongozi

Muktasari:

  • WBaadhi ya waliokuwa makada wa Chadema kabla ya kujiunga na Chaumma, ni sehemu ya Kamati Kuu ya Chaumma baada ya kuteuliwa kwenye nafasi nyeti za uongozi katika chama hicho.

Dar es Salaam. Kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) kinachohusisha wajumbe 15, tayari kimeshaanza katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kinaongozwa na mwenyekiti wa chama, Hashimu Rungwe na kitakuwa kinajadili ajenda kuu mbili ikiwemo kuchagua wakurugenzi wa idara makao makuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ibara ya 55.

Idara zinazotakiwa kupata viongozi ni Habari, Sheria, Uchaguzi na Ulinzi, Idara za Uchumi Fedha na Mipango, Uhusiano na Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa.

Pia, idara nyingine zinazotakiwa kujazwa ni Kamati Kuu ni Mafunzo na Elimu kwa Umma, Idara ya viongozi wa wakilishi wa wananchi kupitia chama na idara ya Sheria, Katiba, Haki za Binadamu na Maendeleo ya Jamii.

Ajenda nyingine inayoangaziwa katika kikao hicho ni kujadili na kupitisha ratiba ya ziara ya kitaifa ya C4C (Chaumma For Change) inayotarajiwa kuzinduliwa jijini Mwanza Mei 30, 2025 ikiwa na lengo la kutambulisha viongozi wapya wa ngazi ya taifa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Salumu Mwalimu, ziara hiyo baada ya kuzinduliwa itazunguka nchi nzima kwa siku 16 mfululizo kwa kutumia usafiri wa chopa.

Watazunguka kupita kutambulisha uongozi wa kitaifa na kupokea wanachama wapya, kueneneza sera za chama na kukiandaa chama kushiriki uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu.

Uchaguzi ambao Mwenyekiti Rungwe amesema safari hii wanaenda kushindana na si kushiriki kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Mbali na Rungwe, wengine waliohudhuria kikao hicho ambacho ajenda zake zilianza kuandaliwa tangu juzi ni Makamu mwenyekiti Tanzania Bara, Devotha Minja, Katibu Mkuu, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Benson Kigaila.

Wengine ni Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa chama hicho na Makamu Mwenyekiti Tanzania Zanzibar.