Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpina amwambia Rais Samia jimboni wanamdai, mwenyewe amjibu

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina

Muktasari:

  • Mpina ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Juni 17, 2025, wakati wa mkutano wa hadhara unaofanyika Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Rais Samia mkoani humo.

Dar es Salaam. Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amemwambia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa jimbo lake bado linamdai fedha za maendeleo na kwamba maeneo mengine yanayodai hayamdai, fedha zao zihamishiwe Kisesa.

Mpina ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Juni 17, 2025, wakati wa mkutano wa hadhara unaofanyika Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Rais Samia mkoani humo.

Katika hotuba yake, Mbunge huyo amegusia pia changamoto ya ununuzi wa pamba kwa kutumia mnunuzi mmoja, akisema kuwa hali hiyo inapunguza ushindani na inazua matatizo iwapo mnunuzi huyo atapata changamoto za kifedha.

“Ombi la tatu Mheshimiwa Rais, suala la mnunuzi mmoja wa pamba linakwamisha ushindani. Na kule Kisesa bado tunakudai. Wanaosema hawakudai, hawakudai zile fedha zihamishwe zije zote Kisesa sababu bado tuna mipango mingi ya maendeleo katika maeneo yetu,” amesema Mpina.

Pamoja na hayo, ametoa pongezi kwa Rais kwa kuunda tume ya maboresho ya kodi, akisema hatua hiyo inaleta matumaini ya kutatua changamoto sugu katika mfumo wa kodi nchini.


Samia amjibu 

Rais Samia Suluhu Hassan amejibu hoja za Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, aliyesema jimbo lake linamdai, akisema kwamba mbunge huyo anaonekana kutumikia Taifa zaidi badala ya jimbo lake kwa kushindwa kuzungumzia masuala ya maendeleo ya jimbo hilo na badala yake anajitafutia umaarufu.

“Ndugu zangu, maombi kama haya yamekwishawasilishwa bungeni na mawaziri wakatekeleze. Kuleta maombi haya hapa kwenye mkutano wa Rais ni kujitafutia umaarufu na kuthibitisha kuwa Mbunge hakulifanyia haki jimbo lake,” amesema Rais Samia 

Rais Samia amesisitiza kuwa Mbunge anapaswa kutumia nafasi yake bungeni kutatua changamoto za wananchi badala ya kuzipigia kelele hadharani. Aidha, amekumbusha kuwa jimbo la Kisesa limepata maendeleo makubwa, kinyume na madai ya mbunge wake.

“Mbunge wa Kisesa anasema jimbo lake halina maendeleo, lakini rekodi za Serikali zinaonyesha kinyume chake. Hii ni kuonesha udharau kwa jimbo lake,” amesema Rais Samia huku akiwataka wananchi kuwachagua wabunge watakaoleta huduma za kweli badala ya siasa za kujitafutia umaarufu.


Endelea kufuatilia Mwananchi.