Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge ahoji kukamatwa kwa Lissu

Muktasari:

  • Katika mchango wake bungeni, Mbunge huyo amesema Chadema wanachotaka (reforms) ni kile ambacho hata Rais Samia Suluhu Hassan anakitaka lakini inashangaza wanapokamatwa na kuwekwa ndani.

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest amehoji sababu za kuwekwa ndani kwa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu wakati anataka mabadiliko.

Anatropia ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumanne Aprili 22, 2025 wakati akichangia kwenye Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi iliyowasilishwa Aprili 16, 2025.

Katika mchango wake, mbunge amesema Chadema wanachotaka ni kile ambacho hata Rais Samia Suluhu Hassan anakitaka lakini inashangaza wanapokamatwa na kuwekwa ndani.

Lisu anashikiliwa gerezani kwa tuhuma za uhaini kutokana na kauli zake wakati akiendelea na mikutano ya chama chake katika mikoa mbalimbali nchini.

Amezungumzia R nne za Rais (maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga upya), akisema ile ya tatu ndiyo ambayo chama hicho kikuu cha upinzani kinaisimamia lakini cha kushangaza kuna watu hawataki kusikia.

“Hivi kama watu wanataka reforms (Mageuzi) kuna shida gani hadi mnamuweka ndani Lisu (Tundu), Simba na Yanga ziko uwanjani halafu unaruhusu refa wa Yanga akachezeshe gemu,” amehoji Anatropia.

Mbunge wa Viti Maalum, Anatropia Theonest akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Ncho Ofisi ya Rais Tamisemi iliyowasilishwa leo Aprili 16,2025 bungeni, Dodoma. Picha na Hamis Mniha

Mbunge huyo amesema ni muhimu haki ikatendeka katika uchaguzi kwa sababu hakuna kitu ambacho wanakitafuta watu kama siyo haki, hivyo lazima wakubali mabadiliko.

Amesema haiwezekani kwenye uchaguzi upande mmoja wakawa na msimamizi na mwamuzi katika watu wanaogombania kitu kimoja.

Anatropia amesema tunu ya Watanzania wanayoitaka ni haki hivyo akawaomba upande wa chama tawala kuwa watulivu kwani hofu yao inatoka wapi ikiwa wamefanya vizuri kwenye maeneo ya maendeleo kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Nkasi Kaskazini Aida Khenani amesema ni aibu kwa Taifa shule za msingi kununua picha ya Rais na Bendera ya Taifa badala ya kuzigawa bure.

“Lakini niseme ukweli na mimi ni Mkristo Mkatoliki, kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa yalifanyika mambo ya hovyo kabisa,” amesema Khenani.

Khenani amesema kilichotokea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kulitokea mambo ya ajabu ambayo maumivu yake ni makubwa hadi sasa.

“Ni aibu ya Taifa, amani ilitengenezwa kwa gharama kubwa hivyo tusione aibu kujisahihisha na kusema tulikosea ili tukubali kulinda amani na haki kwani ndiyo tunda la amani,” amesema Khenani.

Mbunge huyo mbali na msimamo wa Chadema kuwa hawatagombea, lakini ametangaza kuwa anakwenda kujiuliza kwa wananchi kwani wao ndiyo wenye kusema arudi bungeni au abaki.