Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lissu: Matatizo ya Watanzania yana uhusiano na mfumo mbovu wa uchaguzi

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu anaendelea na ziara yake katika maeneo mbalimbali nchini akizungumza na wananchi kuhusu kampeni ya chama hicho ya “No Reforms, No Election”.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema matatizo mengi yanayowakabili Watanzania yana uhusiano mkubwa na mifumo mibovu ya uchaguzi ambayo inazalisha viongozi wasioshughulika na changamoto zao.

Lissu amebainisha hayo leo Machi 29, 2025 wakati akihutubia mkutano wa hadhara huko Makongorosi, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wakati akizungumza na wananchi kuhusu kaulimbiu ya Chadema ya “No Reforms, No Election”.

Amesema wachimbaji wa madini wameongezewa mzigo wa kodi kupitia taasisi mbalimbali zinazokusanya mapato. Pia, amesema wafanyakazi wa nchi hii kama vile walimu, wauguzi, askari polisi wameongezewa mzigo na Serikali kupitia makato wanayokatwa na Serikali.

 “Sasa, matatizo yote haya yana uhusiano na uchaguzi. Kwa nchi yetu, uchaguzi ni namna pekee ya kupata viongozi. Hawa mawaziri wanaotuletea matatizo ni wabunge, ili uwe mbunge lazima uchaguliwe,” amesema.

Amesisitiza kwamba Tanzania ikiwa na mifumo mizuri ya uchaguzi, watapatikana viongozi wazuri watakaotatua shida za wananchi badala ya kuziongeza. Amesema mfumo wa uchaguzi ni muhimu kwa wananchi kulifahamu na kulifanyia kazi.

Lissu amesema mfumo wa uchaguzi hauwaruhusu Watanzania kuchagua viongozi wanaowataka kwa sababu mbalimbali ikiwamo kuzuia mawakala wa Chadema.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema haitakiwi watu kuumizwa ili mbunge wa Chadema atangazwe kuwa mshindi, bali iwe ni utamaduni kwa mshindi kutangazwa bila shuruti.

“Walimu tendeni haki, mnapopata majukumu mnyooke, kimsingi hatutaki nyie msimamie, tunataka mfumo mpya ambao utaondoa watu ambao wanadai walilazimishwa,” amesema Sugu wakati akihutubia wananchi hao.