Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lema apewa jukumu kuiongoza Chadema Kanda ya Kati

Muktasari:

  • Chadema imemtaja Lema kwamba amepewa kazi maalumu ya kuimarisha chama hicho Kanda ya Kati.

Dodoma. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemteua Godbless Lema kuongoza Kanda ya Kati.

Chadema imemtaja Lema kwamba amepewa kazi maalumu ya kuimarisha chama hicho Kanda ya Kati ambacho kwa muda kimekuwa kikisuasua kutokana na kinachotajwa kuwa na uongozi usiofaa.

Akihutubia kwenye mkutano wa wananchi na wanachama wake katika viwanja vya Mtekelezo leo Jumapili Mei 24, 2026, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Unguja, Hashim Juma amemtaja Lema kama jabali la siasa.

Hashim amesema Lema amepitishwa na Kamati Kuu ili aimarishe kanda hiyo inayoundwa na mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Godbless Lema akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jijini Dodoma. Picha na Said Khamis

Nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati imekosa mtu maalumu tangu mwenyekiti wake, Lazaro Nyalandu alipojiuzuru na kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM).

Baada ya Nyalandu kujiuzulu, nafasi yake ilishikiliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Asha Luja ambaye muda wote amekuwa akiishi Marekani.

Kwenye uchaguzi uliopita, Devotha Minja alichaguliwa kuwa mwenyekiti lakini baadaye akatimkia Chaumma ambako alikuwa mgombea mwenza wa kiti cha Rais na baadaye akapata nafasi ya ubunge viti maalumu.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Godbless Lema akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jijini Dodoma. Picha na Said Khamis

“Tunamtangaza Lema hadharani bila kificho kwamba anakuja kuongoza kanda hii, amekuja kwa kazi maalumu ya kuimarisha chama, atakuwa na watu imara wa kumsaidia,” amesema Hashim.

Ujio wa Lema utakuwa ni sehemu ya mtihani kwa chama hicho ambacho Mkoa wa Dodoma hakijawahi kushinda kiti cha ubunge licha ya Singida na Morogoro walishawahi kupata viti vitatu kwa jumla wao.