Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamati Kuu ACT Wazalendo kujifungia kujadili hali ya kisiasa

Wajumbe wa kamati ya uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo, wakiwa katika kikao kilichofanyika Jumatano Aprili 29, 2026 katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho Vuga mjini Unguja.

Muktasari:

  • Naibu Katibu wa Habari na Mawasiliano wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo amesema katika kikao hicho, kitakachoongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Othman Masoud Othman kitapokea taarifa kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea nchini, Bara na Zanzibar na kutoka na maazimio.

Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo, kesho Jumapili Mei 3,2026 itakutana kwa dharura kujadili hali kisiasa inayoendelea nchini.

Kwa mujibu taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Mei 2, 2026 na Naibu Katibu wa Habari na Mawasiliano, Shangwe Ayo imeeleza kuwa kikao hicho kitafanyika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Magomeni Dar es Salaam.

Shangwe amesema katika kikao hicho, kitakachoongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Othman Masoud Othman kitapokea taarifa kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea nchini, Bara na Zanzibar na kutoka na maazimio.

Kikao cha Kamati Kuu hicho, kilitanguliwa na kikao cha Kamati ya Uongozi kilichofanyika Mjini Unguja kilichojadilia masuala mbalimbali ambayo yatafikishwa mkutano wa kesho kwa hatua zaidi za utekelezaji.

Miongoni mwa ajenda ambazo huenda zikajadiliwa katika kikao hicho cha kesho ni suala la Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ambalo linaelezwa kuwa limefikia hatua nzuri ya pande mbili za CCM na ACT Wazalendo kutoka hadharani kueleza umma walivyokubaliana.

Mazungumzo ya kutafufuta mwafaka wa kisiasa Zanzibar, yanaongozwa na Othman Masoud Othman na Juma Duni Haji kwa ACT Wazalendo, huku CCM ukiwakilishwa na marais wastaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Ali Mohamed Shein.

Machi 14, 2026 Othman ambaye ni mwenyekiti wa ACT Wazalendo aliwaondoa wasiwasi Wazanzibari, akiwataka kuwa watulivu kwa kuwa mazungumzo ya kuleta suluhu ya kisiasa Zanzibar yanaendelea vizuri.

Aprili 30, Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita alisema kamati maalumu inayosimamia majadiliano hayo Othman bado inaendelea na jukumu hilo kama ambavyo ilielekezwa na kamati kuu ya chama hicho.

“Jumapili tutakuwa na Kamati Kuu nyingine ni maalumu kwa ajili ya masuala mengine, kama kamati ya SUK itakuwa na cha ‘kubrief’ basi itatoa mrejesho.

“So far tumefika ambapo kamati ya SUK imesema wamefikia hatua ya makubaliano ya kutambua mambo gani ya msingi yanayopaswa kufanyiwa kazi,” ameeleza Mchinjita.