Grace Kiwelu, Mgonja, Kilawila, Rachael wajiondoa Chadema

Moshi. Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kilimanjaro akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Gervas Mgonja, wametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kuanzia leo Jumapili, Mei 11, 2025.

Gervas Mgonja, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro
Wengine waliojivua uanachama ni Katibu wa Bawacha Kanda ya Kaskazini, Rachael Sadick, Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Kiwelu, Mjumbe wa Kamati ya Tehama Kanda ya Kaskazini, Answary Kimaro na Mwenyekiti mstaafu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Michael Kilawila

Baadhi ya viongozi waliojivua uanachama wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Kanda ya Kaskazini
Makada hao ambao wengine wamepata kuwa wabunge, wametangaza uamuzi huo leo, Mei 11, 2025 mjini Moshi, wakati wakizungumza na waandishi wa habari.

Rachael Sadick, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bawacha Chadema Kanda ya Kaskazini
Miongoni mwa sababu walizozitaja kujiondoa Chadema ni madai ya kutokusikilizwa, viongozi kushindwa kukemea matusi yanayotolewa na baadhi ya wajumbe wa chama hicho.
Endelea kufuatilia Mwananchi digital kwa taarifa zaidi.