Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chaumma: Achaneni na CCM ili msiote vipara

Muktasari:

  • Chaumma yadhamiria kuimaliza CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba huku ikisisitiza wananchi kuachana na chama hicho.

Mafinga. Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), kimesema ugumu wa maisha waliyonayo Watanzania unatokana na uongozi wa miaka mingi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Chama hicho kimesema watu hawana nuru wanashindwa hata kupaka mafuta kwa sababu ya ugumu wa maisha.

Maneno hayo yametolewa na Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Chaumma, Devotha Minja wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika jimbo la Mafinga uwanja wa Shule ya Msingi Mkombwe Iringa.

"Watu wamechoka hata mafuta hawapaki vijana wanajikuna vichwa, wanaupara kwa sababu ya mawazo yanayosababishwa na maisha magumu yote kisa CCM," amesema.

Akieleza zaidi amesema Tanzania ni tajiri wa rasilimali ikiwemo madini ya kila namna, bandari, ardhi inayostawisha mazao mbalimbali, lakini wananchi bado wanamaisha magumu.

Akieleza mkakati amesema watatumia bandari zilizopo, mabonde ya maji na ardhi nzuri kwenye kilimo ili Watanzania wapate maisha mazuri, ikiwemo kuwapatia ubwabwa  wakienda hospitalini na shuleni vyakula viwe bure.

"Ni wakati wa CCM kupumzika, Chaumma tutalala nao kiulalo ulalo. Tutaenda nao bampa tu bampa hadi kieleweke.

"Kwanza wanaosema sisi sio CCM B, niwaulize hivi wewe ukienda kununua kuku utamuweka kwenye banda lako au la jirani? Sasa CCM watununue sisi watupeleke Chaumma si wangetupeleka CCM kwani hawaoni nguvu zetu?

"Kwani tulipokuwa Chadema hatukuwa tunarusha chopa. Ilikuwa inaruka. Mbona walikuwa hawaulizi. Kurusha chopa ni vichwa tulivyokuwa navyo kule tumekuja navyo huku," amesema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chaumma Zanzibar, Mohammed Masoud Rashid amesema mwaka huu jino kwa jino na CCM hadi wawang'oe madarakani.

Amesema katika kuwang'oa CCM hawapaswi kususia uchaguzi bali wakubali mabadiliko ili kusudi wapate maendeleo.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimesema kitapambana kwenye sanduku la kura katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu hadi kiitoe Chama tawala CCM.

Chama hicho kinasema hayo wakati ikiwa imesalia karibu miezi mitatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu.

Katika kukabiliana na CCM chama hicho kimesema wananchi waunge mkono upinzani wenye nguvu kwakuwa adui yao ni CCM.

Ziara ya Chaumma for Change ‘C4C’ ambayo ni mzunguko wa pili ikiwa lengo la kukiandaa chama kuelekea uchaguzi mkuu pili, kutambulisha safu ya uongozi wa kitaifa, kuweka uongozi katika baadhi ya mikoa na kupokea wanachama wapya wanaojiunga.

C4C ilizinduliwa mwaka huu 2025 katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza na baada ya hapo ilizunguka katika mikoa iliyopo kwenye kanda nne za Serengeti, Victoria, Kaskazini na Magharibi.

Kwa sasa ziara inaendelea katika mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Tanga, Iringa na Njombe kikieleza sera zake.