Kada wa CCM atimkia Chaumma
Biharamulo. Aliyekuwa Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Peter Buhime amejiunga rasmi na Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), na kukabidhiwa kadi na Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Umma wa Chaumma, John Mrema katika Mji wa Biharamulo.
Peter, aliyewahi kuwa mtia nia wa Ubunge Jimbo la Biharamilo kupitia CCM mwaka 2020. Kada huyo pia amewahi kuwa Katibu wa UVCCM, Kata ya Saranga, Kibamba jijini Dar es Salaam.
Endelea kufuatilia Mwananchi.