Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Patrice Lumumba: ‘Mbega’ aliyeponzwa na manyoya yake

Muktasari:

Lumumba ambaye alifanikiwa kuzima uasi wa kujitenga kwa majimbo kadhaa nchini mwake yakiwamo Katanga, Kasai, alionekana dhahiri kuwa mwiba kwa watawala wa zamani wa nchi ile.

Ni miaka 53 imepita tangu kufanyika kwa mauaji ambayo unaweza kuyaita ni mabaya kwenye karne ya 20.

Januari 17, 1961, dunia ilishuhudia mauaji ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC), Patrice Emery Lumumba.

Mauaji hayo ambayo yalifadhiliwa na Marekani na Ubelgiji yalitokea mwaka mmoja baada ya Kongo kupata uhuru wake.

Lumumba, aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa kuchaguliwa wa nchi hiyo, mauaji yake yamebakia yenye kukumbukwa.

Wataalamu wanaeleza kuwa yalipangwa na Marekani na Ubelgiji na kutekelezwa na kikosi maalum cha wauaji.

Mwandishi wa vitabu, Ludo De Witteu, raia wa Ubelgiji anayaita mauaji hayo “maarufu karne ya 20’.

Pia, mauaji ya Lumumba yana umuhimu mkubwa katika historia ya DRC hadi sasa.

Yamekuwa yakifuatiliwa kwa jinsi yalivyotekelezwa na kisha kuiachia doa nchi hiyo hadi leo kisiasa, kiuchumi.

Kwa miaka 126, Marekani na Ubelgiji zimekuwa na sauti kwenye uhai wa Kongo kama nchi baada ya mkataba wa kimataifa wa Berlin mwaka 1884.

Miezi saba kabla ya mkataba huo, Baraza la Congress la Marekani lilitambua madai ya Mfalme Leopold II wa Ubegiji kwamba Bonde la Mto Kongo lilikuwa mali yake.

Masilahi ya kiuchumi ya Wabelgiji na Wamarekani nchini Kongo ndiyo yaliyochochea mauaji ya Lumumba, mtu ambaye alisimama kidete na kupingana nayo.

Upinzani wa Lumumba kwa wakoloni hao ulionekana dhahiri kuwa tishio kwao, ndiyo maana alipoingia madarakani wakubwa walichukizwa na hivyo kusaka mbinu ya kumwangamiza.

Lumumba ambaye alifanikiwa kuzima uasi wa kujitenga kwa majimbo kadhaa nchini mwake yakiwamo Katanga, Kasai, alionekana dhahiri kuwa mwiba kwa watawala wa zamani wa nchi ile.

Ubabe wa watawala wa Ubelgiji chini ya Mfalme Leopold II kwa kiasi kikubwa ulisababisha mauaji ya watu wengi katika nchi hiyo huru, jambo ambalo Lumumba alipingana nalo kwa nguvu na akili zake zote. Matokeo yake, Lumumba alionekana adui na tishio kwa usalama wao, kiasi cha wakubwa hao kupanga namna ya kumwangamiza mapema kabla ya kufika mbali katika dhamira yake ya kuhakikisha kuwa unyonyaji wao unaondolewa. Madini ya urani kutoka Kongo ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo yaliyotumika kutengeneza bomu la nyuklia ambalo lilipiga miji ya Nagasaki na Hiroshima nchini Japan ndiyo yaliyomwingiza Lumumba kwenye mzozo na wakubwa hao. Vita baridi vya wakati ule na msimamo wa Lumumba akionekana kuungwa mkono na wakubwa kama Urusi, ilikuwa sababu ya kuwindwa kwake, hatimaye kuuawa.

Ndiyo maana Marekani na Ubelgiji zikatumia kila mbinu na rasilimali na vyombo vingine kama sekretarieti ya Umoja wa Mataifa (UN) chini ya Dag Hammarskjold akiwa Katibu Mkuu na Ralph Bunche kuwanunua wabaya wa Lumumba, kisha kuwaajiri wauaji. Wengi katika DRC hadi leo bado wanaamini mauaji ya Lumumba kuwa chanzo cha mabaya ambayo yanaisibu nchi hiyo hadi leo. Ni dhambi ya asili ya DRC, mauaji ambayo yalifanyika miezi saba baada ya uhuru wa nchi hiyo, Juni 30, 1960, ambayo yameendelea kuwa kikwazo cha kupatikana kwa umoja wa kitaifa, ustawi wa kiuchumi na umoja wa Afrika ambao aliupigania Lumumba.

Hadi leo, mamilioni ya raia wa nchi hiyo wamegawanyika. hawana umoja, wenginje ni wakimbizi.

Kifo chake, Lumumba kilitokea wakati migawanyiko ikiwa imeanza katia nchi hiyo changa, hali ambayo imeendelea hadi sasa, inawatesa wanasiasa ambao wamefuata baada ya Lumumba.