Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkongwe wa miondoko ya R&B mwenye muziki usiochuja

Muktasari:

Hilo limechangiwa na sauti tamu na mpangilio mzuri wa maneno ya mahaba yanayoonekana kusheheni kwenye nyimbo zake nyingi.

Licha ya kuwa nyimbo zake nyingi alizitoa miaka ya 90 lakini zinapopigwa mpaka sasa zinaonekana kuwagusa wapenzi wengi wa muziki wenye miondoko ya taratibu.

Hilo limechangiwa na sauti tamu na mpangilio mzuri wa maneno ya mahaba yanayoonekana kusheheni kwenye nyimbo zake nyingi.

Hapa tunamzungumzia mwanadada Celine Dion mkali wa miondoko ya R&B ambaye jina lake linaendelea kusikika kila kukicha licha ya kuwa hajatoa nyimbo mpya katika kipindikirefu.

Kwa wafuatiliaji wa miondoko hiyo lazima watakuwa wanafahamu nyimbo kama Power of Love,I Love You, Immortality, My Heart Will Go On, Because You Loved Me, Love Doesn’t Ask Why na nyinginezo.

Nyimbo hizi zimetungwa na kuimbwa miaka 20 mpaka 15 ilopita lakini mpaka sasa zinapopigwa redioni humfanya msikilizaji kuhamisha mawazo yake kutoka sehemu nyingine na kumsikiliza mwanadada huyu.

Kujipambanua kwake na wanamuziki wengine kumemfanya Celine kutawala miondoko ya R&B kwa mtindo unaomfanya kuendelea kuwa wa pekee.

Kuzaliwa kwake katika familia yenye mwamko mkubwa kwenye muziki huenda ndiyo ilikuwa sababu ya mwanamuziki kukuza kipaji chake ambacho kilianza kuonekane tangu alipokuwa mtoto.

Wazazi wake walianzisha kundi la muziki lililowahusisha familia nzima iliyokuwa na jumla ya watoto 14 kundi lililofahamika kama Dion’s Family.

Celine akiwa mtoto wa mwisho kwenye familia hiyo alionyesha kuwa na mapenzi zaidi na muziki hata alipofikisha umri wa miaka mitano tayari alishaanza kuimba na kupiga piano.

Alipofikisha miaka 12 mama yake alimrekodi sauti yake na kumpelekea mtayarishaji wa muziki Rene Angelil ambaye alionyesha kuvutiwa na sauti hiyo.

Angelil aliagiza Celine apelekwe ili amsikilize mwenyewe na alipomsikiliza hakujiuliza mara mbili zaidi ya kumsainisha mkataba na kuchukua jukumu la kumsimamia kwenye muziki wake.

Huo ndiyo ukawa mwanzo wa safari ndefu ya mwanamuziki huyu ambaye anaweza kuitwa malkia wa miondoko ya R&B.

Umaarufu wake ulishika kasi katika miaka ya 90 alipoachia albamu ya Unison iliyobeba vibao vikali kama ‘Where Does My Heart Beat Now’. Albamu hiyo iliuza zaidi ya nakala milioni moja duniani kote.

Mwaka 1993 aliachia albamu ya ‘The Colour of My Love’ iliyosheheni nyimbo kadhaa za mapenzi zikiwamo When I Fall in Love na Power of Love kibao kilichopokelewa vizuri na wapenzi wa miondoko ya R&B hata kufanikiwa kushika namba 1 katika chati za nyimbo 100 za Billboard.

Akiwa na miaka 26 Celine alifunga ndoa na Angelil ambaye ni meneja wake kwa wakati huo alikuwa na umri mara mbili ya nyota huyo.

Imendaliwa na Elizabeth Edward