Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Teknolojia rahisi ya uzalishaji mbogamboga kwa njia za kisasa

Mjasiliamali akiuza mboga, wataalamu wanasema utunzaji wa mboga kwa njia za kienyeji hushusha ubora wake

Muktasari:

Vipo ambavyo kwa namna vilivyo vinahadharishwa visitumike kwa wingi na vipo ambavyo kwa baadhi ya watu wenye maradhi fulanifulani, inabidi wasivitumie kabisa.

Katika miaka ya karibuni, vyakula vingi vinavyotumiwa na binadamu, vimeonekana kuwa na madhara kwa afya hivyo wataalamu kushauri vitumike kwa tahadhari.

Vipo ambavyo kwa namna vilivyo vinahadharishwa visitumike kwa wingi na vipo ambavyo kwa baadhi ya watu wenye maradhi fulanifulani, inabidi wasivitumie kabisa.

Hii inahusisha vyakula ambavyo ni tegemeo au vimezoeleka kwa jamii kiasi kwamba wengine wamefikia hatua ya kusema hakuna namna, inabidi wavitumie vivyo hivyo, lolote litakalotokea, potelea mbali.

Vyakula kama nyama na mafuta, vimekuwa vikitumiwa enzi na enzi lakini katika miaka ya karibuni vimeonekana ndivyo vinavyochochea matatizo mbalimbali kama vile maradhi ya moyo, kiharusi, lehemu, matatizo ya viungo, uzito kupita kiasi na kisukari.

Chumvi na sukari ni moja ya vitu muhimu ambavyo vinaongeza ladha lakini siku hizi wataalamu wanahadharisha vitumike kwa kiwango cha chini kuepuka maradhi kama vile matatizo ya moyo na kisukari.

Kwa wenye tatizo la shinikizo la damu wanakatazwa kutumia chumvi na wale wenye kisukari hukatazwa kutumia vyakula au vinywaji vyenye sukari.

Wataalamu wanasema ukiangalia vyakula karibu vyote vina mazingira ya kuwekewa masharti ya kutumia kutokana na maradhi fulani.

Pamoja na yote hayo, wanasema pia kuwa mboga za majani ni moja ya chakula ambacho kimeonekana ni bora zaidi kuliko vingine.

Wanasema watu wengi hudharau mboga za majani wakati wa mlo lakini kitaalamu zingepeswa kutumika kwa wingi zaidi.

Taasisi Inayojihusisha na Tafiti za Mbogamboga Duniani (AVRDC) inaamini kuwa, mboga za majani ni moja ya chakula ambacho kitajijengea umaarufu kwa kuwa muhimu zaidi kwa binadamu.

Tasisi hiyo inayoratibu tafiti hizo barani Afrika, inasema tayari nchi zilizoendelea zimeanza kutumia mbogamboga kwa wingi zaidi kwenye milo kuliko aina nyingine za vyakula.

Mratibu wa Mafunzo wa AVRDC Ukanda wa Afrika, Hassan Mndiga anasema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa wanaotumia mboga za majani kwa wingi katika milo yao wanakuwa na uwezo mkubwa katika kujikinga na maradhi.

Anasema ni kutokana na mboga za majani kuwa na viinilishe vingi muhimu kwa mwili wa binadamu na hazina asili ya kuwa na vichocheo vya madhara kama ilivyo kwa vyakula vingine.

Anasema mboga za majani ni dawa kwa watu wenye maradhi mbalimbali kama vile ya ngozi, kuona na viungo.

“Mboga za majani ni dawa. Zikitumika ipasavyo, mtu anaweza kupona na kuepuka maradhi madogomadogo ambayo pengine angeyaacha yangeweza kumletea matatizo makubwa,” anasema Mndiga.

Anasema AVRDC ambayo ofisi zake hapa nchini zipo Arusha, inatambua umuhimu wa mboga na hata kiwango cha uhitaji kwenye soko la dunia ndiyo maana imewekeza katika kuhamasisha uzalishaji wake.

Inachofanya AVRDC ni kuhakikisha wanatumia teknolojia zilizopo duniani kwa sasa ili kuzalisha mbegu boro, kutoa mbinu za uhifadhi wa mazao yake ili zisiharibike na namna bora ya uzalishaji.

Mbegu bora

Mndiga anasema mbogamboga nyingi za asili zinaonekana kupotea kwa kasi kwenye maeneo mengi hapa nchini.

Aina hizo za mbogamboga anasema ni kama vile mchicha, mnavu, nyanya, ngogwe (nanya chungu), shona nguo, bamia, karoto na mgagani.

Anasema kupotea kwa aina hizo za mboga za asili ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, magonjwa na kuzuka kwa wadudu wengi waharibifu.

Kutokana na hali hiyo, anasema wanachofanya AVRDC ni kujaribu kuzalisha mbegu mpya ambazo hazina magonjwa wala si rahisi kushambuliwa na wadudu.

Anasema sheria za kimataifa zinakataza matumizi ya dawa za kuuliwa wadudu hasa kwa jamii ya mbogamboga, hivyo wanachokifanya ni kuhakikisha mbegu mpya zinakuwa bora zaidi.

Kwa namna wanavyotengeneza mbegu mpya, anasema huweza kuchanganya aina mbalimbali za mboga husika na kuzalisha ambazo hazishambuliwi na maradhi au wadudu na zinazozaa zaidi.Anasema kwa kutumia maabara zao wameweza kuzalisha mbegu za mchicha zinazozaa kwa wingi zaidi.

Vilevile katika uboreshaji huo, moja ya mambo wanayozingatia anasema ni kuhakikisha zinakuwa na ladha za asili.

Anatoa mfano wa bamia za kienyeji na kigeni zinazolimwa nchini.

“Aina zilizo bora zaidi, kuna zenye miiba na zisizo na miiba, pia kuna zenye migongo na zisizo na migongo,” anasema Mndiga.

Ulimaji

Mndiga anasema kuwa mbogamboga ni moja ya mazao ambayo mkulima anaweza kupata faida kubwa katika eneo dogo iwapo atafuata kanuni za kitaalamu.

Anatoa mfano wa mbegu wanazozalisha, akisema ni zile zilizolenga mkulima kupata mazao mengi katika eneo dogo na kwa kutotumia gharama kubwa kama vile dawa za kuulia wadudu na mbolea za kisasa ambazo zina kawaida ya kuongeza kemikali ardhini.

Vile vile, anasema mbegu wanazozitengeneza ni zile ambazo zinatoa mazao ambayo yanaweza kudumu kwa muda mrefu bila kuharibika hasa zinapozingatiwa taratibu za uhifadhi.

“Njia inayotumika ni ya kimaabara ambapo njia za kitaalamu za kusafisha na kuboresha vinasaba,” anasema.

Anasema kila aina ya mbogamboga ina namna yake ya upandaji na utunzaji na kwamba wanachokifanya ni kuhakikisha wakulima wanakuwa na elimu sahihi kulingana na aina anayotaka kulima.

Kwa kuwa mboga zimeonekana kuwa na manufaa mengi, anashauri kila familia kuwa na utaratibu wa kuotesha mboga za majani hata sehemu ndogo kwa ajili ya familia.

Uhifadhi na uuzaji

Anasema mbogamboga ni zao linaloharibika kwa haraka zaidi kuliko mengine.

Hivyo kinachohitajika ni mkulima kuhakikisha kwamba mazao yake yanafika sokoni yakiwa katika hali nzuri na inayokubalika kimataifa.

Pamoja na mbegu wanazozalisha kutumia teknolojia inazoziwezesha kudumu kwa muda mrefu baada ya kuvunwa, mkulima anapaswa kuwa muangalifu.

Uangalifu huo, anasema unaanzia anapovuna, uhifadhi, vyombo vya kusafirishia na muda tangu zinapovunwa hadi kumfikia mlaji.

Kwa kuwa mazingira ya Tanzania bado ni duni na si rahisi kutumia njia za kisasa za uhifadhi kama vile majokofu yenye kiwango cha ubaridhi unaodhibitiwa, inabidi kutumia njia za kienyeji.

Namna ya uvunaji bora, anasema inatofautiana na ni ya mbogamboga lakini maelekezo yake ni yale ya kufanya mazao hayo kumfikia mlaji yakiwa katika hali ile ile ilivyokuwa shambani.

Mfano kama ni mchicha, unapaswa ufike sokoni ukiwa haujanyauka na hata namna ya kuuweka kusubiri mlaji iwe ni ile ile ya kuendelea kudhibiti usiharibike.

Njia za kienyeji ni pamoja na mazao kufunikwa na majani kama vile ya migomba, kunyunyiziwa maji na kama ni nyanya zikishavunwa hupangwa vizuri kwa kuelekeza kovu chini.

Kwa zile mbogomboga zinazozosafirishwa nje ya nchi, Mndiga anasema zinahitaji kufugwa vizuri.

Anasema Afrika ni eneo ambalo linaweza kufanywa kama eneo maalumu la kuilisha dunia kwa mazao ya mbogamboga kutokana na mazingira yake ya eneo kubwa kuwa la kitropiki.