Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unawajua  wake ngumi mkononi au ndoo ya taka?

Muktasari:

  • Mara nyingi kwenye ndoa kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wanaume, na malalamiko haya yanaelekezwa kwenye namna wake zao wanavyoishi au wanavyofanya.

Mara nyingi kwenye ndoa kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wanaume, na malalamiko haya yanaelekezwa kwenye namna wake zao wanavyoishi au wanavyofanya.

Huyu analalamika mke wangu yuko hivi, na yule naye anasema mke wangu yuko vile. Mmoja anasema mke wangu anafanya hivi na mwingine analia mke wangu hafanyi vile.

Huu mkanganyiko umekuwa mkubwa sana na unasababaisha maumivu na migongano kwenye ndoa nyingi.

Hii ndio sababu nimeamua kuandika  makala haya itakayokusaidia kufahamu kuwa wake zetu pamoja na kwamba wanafanana kijinsi,  lakini kwenye tabia zao katika ndoa wanatofautiana.

Kwa mwanamke, pengine  kwa kuisoma makala haya utajigundua kuwa wewe ni mke wa aina gani. Nakutakia usomaji mwema.


Mke sherehe

Wake wa aina hii wako mguu na njia kila siku na wanajuana na kila mtu. Wao kila siku wana sherehe, leo sendoff, kesho kichen party, keshokutwa bag party,  mtondogoo wedding party.

Mara chache wanakaa nyumbani. Zile siku ambazo mume na watoto wapo nyumbani,  yeye ndio hamu ya kutoka inapanda. Wanaweza kutumia hela ya chakula cha familia kuchangia sherehe au kununulia zawadi.   


Mke kamusi

Haihitaji kuomba ushauri hata siku moja yeye anachojua ndio mpango mzima. Kila wakati analazimisha mawazo yake yawe sawia na yaaminike.

Hataki kupingwa au kurekebishwa kwa chochote. Anatoa oda tu, neno naomba au tafadhali hutolisikia kwake, na ni mkali sana vitu vinavyopotea au kuwekwa vibaya nyumbani tofauti na alivyovipanga yeye.  

Mke pampasi 
 

Huyu ni mke aliyeharibiwa kabisa na wazazi wake hususani wazazi matajiri, wazazi wanaojiweza, au labda ndio binti pekee kwao. Wavivu sana kufanya kazi za nyumbani. Wao wanapenda tu kununuaa na vitu vya fasheni. Mara nyingi mke huyu anamuona mume wake kama house boy, utasikia baby nisaidie hiki, baby niletee kile.

Mke ofisi
Mke wa aina hii anajali sana majukumu ya kazini kuliko familia yake, anaweza kuwa na muda mrefu sana wa kazi akakosa muda na watoto au mume wake na anatumia majukumu ya kazi kama kisingizio cha kutokuwepo nyumbani au kutotimiza majukumu yake ya mke au mama nyumbani. 

Ni ngumu sana kwa mke wa hivi kumheshimu mume wake, na hawa ndio wanaowafanya wanawake wengine waliosoma kuonekana wabaya kwenye ndoa.

Mawazo yao ni kwamba mume hana umuhimu sana maana hata wao wanaweza kuendesha familia bila shida. Waume wanaoishi na wake wa aina hii wanastahili pole.


Mke mgonjwa  
 

Wakati wote anaonekana kama anaumwa, mpole sana na aliyenyong'onyea.  Anapenda kulaumu kila kitu, atalaumu kuhusu mume, watoto, ndugu hata hali ya hewa.

Kila wakati wao ni wenye hofu kwa kila kitu, ukimshauri afanye biashara hii anaogopa mwambie nyingine ataogopa, anaweza kulalamika uchovu au kuumwa hata katika nyakati mume anaomba tendo la ndoa.

Pamoja na lawama za udhaifu na kuumwa au kuchoka mara kwa mara,  wala hauoni akisema anaenda hospitali.   


Mke mwalimu mkuu
 

Hawa hujiweka kuwa viranja wa familia hata kama mume ndio anayeleta kila kitu. Kila wakati anatamani aonekane yeye ndio kiongozi wa familia.

Mara nyingi huwafanya wengine wote ni watoto au wanafunzi bila kujali huyu ni mume wake au yule ni mgeni kaja kutembelea familia. Wanauliza maswali kwenye kila kitu, utaskia, kwanini umefanya hivi, kwanini hiki kiko pale, kwanini hivi kwanini vile na pia wanaweza kutoa adhabu hata kwa waume zao kwa vitu visivyo vya maana kabisa.


Mke ngumi
 

Wake wa namna hii ni wenye kuudhi kila mara na pia mara kwa mara ni wapenda fujo. Anaweza kuweka mazingira ya vurugu hata kama haukuwa na mpango wa kurusha ngumi ukajikuta mmekunjana.

 Wanapenda kupayuka sana, atarusha maneno kwa sauti ya juu tena maneno yaliyounganika kama vile taarabu na kama ndio mnaishi uswahilini kila jirani atajua ‘kimenuka’ kwenu..  

Mke ndoo ya taka


Hawa ni wachafu wakati wote na wala hawajipendi kimuonekano, anaweza kuvaa kitu cha gharama lakini bado hauoni kama kavaa kitu. Unaweza kumkuta sehemu ya utanashati sana labda ni sherehe ya watu wazito,  lakini yeye kavaa kikawaida  na wala hajishangai.


Mke mlinzi
 

Wake wa aina hii wanawabana sana waume zao. Wana wivu sana na waume zao. Kwake kila mwanamke ni tishio dhidi ya mme wake, hawamuamini mwanamke yeyote kukaribiana na mume wake, hata mume anapokutana na mwanamke ambaye ni rafiki wa mke wake anahofia kumwambia mkewe kuwa nimekutana na rafiki yako kwa sababu mke atakosa imani kabisa.

Mke wa hivi huwaona marafiki wote wa mume wake kuwa ni maadui na wapotoshaji. Ni wabishi sana kumruhusu mtu mwingine amuadabishe au kumuadhibu mtoto  wake. Hawa ndio wale wanaenda shule haraka sana akiskia mwalimu kamchapa mtoto wake.


Mke mzuri

Huyu ndio yule mke ambaye amezungumzwa kwenye zaburi na vitabu vingine vitakatifu. Anajali, anajua kupenda, anapendeza na anawapenda wa kwake.

 Anaweza kusimamia shuhuli za mumewe asipokuwepo pasipo shida yoyote. Mara zote yeye ni mlinzi na kiongozi wa kiroho kwa watoto na hata familia yote. Ni mwelewa, mwenye ujasiri na anayejiamini.