Takwimu ya watalii wanaofika nchini yapaa

Muktasari:
- Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika kuboresha mazingira ya biashara na uwezekaji nchini sheria na kanuni 66 zimerekebishwa na kufutwa tozo, ada na faini 383.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema idadi ya watalii wa kimataifa wanaofika nchini imeongezeka kwa asilimia 132.1.
Ongezeko hilo ni kutoka watalii 922,692 mwaka 2021 hadi kufikia watalii milioni 2.41 mwaka 2025 huku idadi ya watalii wa ndani nao wakiongezeka kwa asilimia 307.9 kutoka watalii watalii 788,933 mwaka 2021 hadi kufikia watalii milioni 3.218.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Juni 27, 2025 wakati akihutubia Bunge jijini Dodoma ikiwa ni hatua ya kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
“Hatua hii imewezesha vijana wa Kitanzania kupata ajira za moja kwa moja kwenye sekta ya utalii katika vituo na kufungua kampuni zao binafsi za utalii,
Idadi ya wakala wa watalii imeongezeka kutoka 2,885 mwaka 2020 hadi 3,735 mwaka 20225, kwa upande wa waongoza watalii idadi imeongezeka kutoka 576 hadi 7662 mwaka 20205.
Kuhusu mapato yatokanayo na utalii, Rais Samia amesema yamepanda kutoka dola za Marekani milioni 700 hadi 3.9 bilioni mwaka 2024.
Kilichofanyika uwekezaji
Rais Samia amesema katika kuboresha mazingira ya biashara na uwezekaji nchini sheria na kanuni 66 zimerekebishwa na kufutwa tozo, ada na faini 383.
Amesema Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi 2175 katika sekta mbalimbali za uzalishaji na huduma miradi ambayo ina thamani ya dola milioni 25.5.
“Miradi hiyo inatarajia kuzalisha ajira 650,674 za moja kwa moja na ajira nyinginze, jitihada zingine za kuhamasisha uwekezaji maeneo ya uwekezaji imevutia miradi mingine ya uwekezaji 45 yenye thamani ya dola bilioni 1.17 iliyopatiwa leseni la EPZA na EMZ,” amesema.