Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wito vyuo vikuu kutafsiri sera za elimu jumuishi kivitendo

Kituo cha kwanza cha rasilimali kwa watu wenye ulemavu (DIRC) nchini Sudan Kusini, kilichozinduliwa rasmi katika chuo kikuu cha Juba, kinaweza kuwa mfano kwa vyuo vikuu vya Afrika katika kutafsiri sera za elimu jumuishi kuwa vitendo halisi, hasa katika mazingira yenye rasilimali chache.

Kituo hiki kinalenga kuwapa wanafunzi wenye ulemavu fursa sawa ya kupata elimu ya juu ili kuharakisha maendeleo endelevu.

Mtafiti wa Sudan Kusini James Bilal alisema kuanzishwa kwa kituo hicho, ni mfano muhimu kwa vyuo vikuu Afrika vinavyotaka kutekeleza kwa vitendo ahadi za elimu jumuishi.

‘’Kwa kuanzisha rasmi huduma za msaada na hatua za upatikanaji ndani ya mfumo wa vyuo vikuu, DIRC inaonyesha namna taasisi za elimu ya juu zinavyoweza kutoka kwenye sera hadi utekelezaji wa haki ya elimu kwa watu wenye ulemavu, ‘’ alisema.

Aliongeza kuwa ikiwa kitaungwa mkono na kuigwa, kituo hicho kinaweza kusaidia kuongeza usawa katika upatikanaji wa elimu ya juu barani Afrika.

Watu wenye ulemavu nchini Sudan Kusini na Afrika kwa ujumla wanakabiliwa na changamoto kubwa za elimu, hasa kutokana na miundombinu isiyofikika kirahisi na ukosefu wa vifaa vya kujifunzia vinavyokidhi mahitaji yao.


Mfano endelevu Afrika

Bilal alisema uzinduzi wa DIRC ni hatua muhimu katika kuendeleza elimu jumuishi, lakini usawa wa kweli unahitaji dhamira ya kisiasa, rasilimali za kifedha na utekelezaji madhubuti wa sera.

‘’Mtazamo wa haki za binadamu unahitaji sio wanafunzi wenye ulemavu wasikubaliwe tu vyuoni, bali pia wapewe msaada, mazingira rafiki na fursa za kustawi kielimu na kijamii,’ alisisitiza.

Pia alieleza kuwa mifumo ya ufuatiliaji na uwajibikaji ni muhimu kuhakikisha kituo hicho kinatimiza malengo yake na kuwa mfano endelevu.

Kituo hicho kinachangia kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hasa yale yanayohusu elimu, ajira, usawa na upatikanaji wa huduma.

Kwa mfano, lengo la nne linahakikisha elimu bora na jumuishi kwa wote ifikapo mwaka 2030, huku malengo mengine yakihimiza ukuaji wa uchumi, kupunguza pengo la usawa na kuboresha mazingira ya makazi.

Bilal alibainisha kuwa wanafunzi wenye ulemavu bado wanakabiliwa na vikwazo kama miundombinu isiyofaa, uhaba wa teknolojia saidizi, vifaa vya kujifunzia kama mashine za nukta nundu na wakalimani wa lugha ya alama.

Aidha, unyanyapaa na uelewa mdogo kuhusu haki za watu wenye ulemavu huendelea kuchochea kutengwa kwao.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2023, takriban asilimia 16 ya watu nchini Sudan Kusini wanaishi na ulemavu, hali inayochangiwa na migogoro, umaskini na huduma duni za afya.

Hata hivyo, Bilal alionya kuwa utekelezaji wa DIRC unaweza kukumbwa na changamoto kutokana na uwekezaji mdogo wa serikali katika sekta ya elimu.

Kwa mfano, mwaka wa fedha 2024/25, elimu ilipata asilimia 2.7 tu ya bajeti ya taifa, hali inayopunguza upatikanaji wa wataalamu na teknolojia muhimu.

Kutokana na hali hiyo, uendelevu wa miradi kama hii unaweza kutegemea msaada wa nje.

Alisisitiza kuwa ni muhimu kuongeza uwekezaji, kuboresha mafunzo ya walimu na kushirikisha wadau mbalimbali ili kuhakikisha mafanikio ya muda mrefu.

Makala haya kwa yametafsiriwa kutoka mtandao wa universtyworldnews.com.