Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hispania yaivua Argentina ubingwa wa Dunia

Muktasari:

  • Hispania imetwaa ubingwa wake wa pili katika historia ya Kombe la Dunia ikiwavua mabingwa watetezi Argentina.

Hispania imeandika historia mpya katika soka baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2026, ikiivua Argentina iliyokuwa bingwa mtetezi kwa ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa hadi dakika 120.

Shujaa wa La Roja alikuwa mshambuliaji Ferran Torres aliyefunga bao la ushindi dakika ya 106 kwa mguu wa kushoto, akimalizia pasi ya kichwa kutoka kwa Nico Williams na kuwapa Wahispania taji la pili la dunia.

Dakika 90 za mchezo huo zilikamilika bila timu yoyote kufunga, huku Hispania ikiwa na udhibiti mkubwa wa mchezo na kutengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga.

Hispania ilifanya mashambulizi 16 yaliyolenga lango la Argentina, huku 11 yakizuiwa na kipa Emiliano Martínez aliyekuwa nguzo muhimu kwa mabingwa hao wa zamani kwa kuokoa michomo hatari.

Kwa upande mwingine, Argentina ilishindwa kuonyesha makali kwenye safu yake ya ushambuliaji, ikicheza dakika zote 120 bila kupata shuti lililolenga lango.

Hispania ilikuwa ya kwanza kutishia lango dakika ya nne, baada ya mshambuliaji Lamine Yamal kupiga shuti lililozuiwa na mabeki wa Argentina kabla ya Martínez kuokoa hatari hiyo.

Argentina ilijibu dakika ya sita baada ya Lionel Messi kupata nafasi nzuri, lakini kipa Unai Simón alitoka kwa wakati na kumzuia mshambuliaji huyo asiingie kwenye eneo la kufunga.

Dakika ya 38, Mikel Oyarzabal alipata nafasi nzuri nje kidogo ya eneo la hatari, lakini shuti lake kali liliokolewa na Martínez.

Argentina ilipata pigo kabla ya kumalizika kwa mchezo baada ya kuwapoteza mabeki wake wawili, Lisandro Martínez na Cristian Romero, waliotoka kutokana na maumivu, lakini timu hiyo iliendelea kuonyesha nidhamu kubwa ya ulinzi.

Katika dakika za nyongeza, Argentina ilipata pigo lingine baada ya kiungo Enzo Fernández kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90+3 kufuatia kupata kadi mbili za njano ndani ya muda mfupi.

Ushindi huo umeifanya Hispania kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya pili katika historia yake, baada ya mafanikio ya kwanza mwaka 2010 kwenye fainali zilizofanyika Afrika Kusini, ambako pia ilishinda kwa bao 1-0.