Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

IITM wajitosa kutoa elimu ya Akili Mnemba

Profesa Raghunathan Rengaswamy, wa IIT Madras, India akitoa mhadhara kuhusu matumizi ya Akili Mnemba katika diplomasia

Dar es Salaam. Wakati matumizi ya Akili Mnemba (AI) yakikithiri duniani huku baadhi wakiwa na hofu nayo, Taasisi ya Teknolojia ya Madras ya nchini India (IITM) kampasi ya Zanzibar imejitosa kutoa elimu yake kwa kina.

Akizungumza kuhusu suala hilo katika hafla iliyowakutanisha wanadiplomasia mbalimbali visiwani Zanzibar, Mkuu wa Kitengo cha Mwingiliano wa Kimataifa wa chuo hicho, Profesa Raghunathan Rengaswamy, amesema:

“AI inaweza kuwasaidia wanadiplomasia kuelewa mienendo ya kimataifa vyema kupitia uchanganuzi wa hali ya juu wa data na taarifa mbalimbali za kitaifa na kimataifa.”

Hafla hiyo ya mafunzo kwa wanadiplomasia ilifanyika Desemba 4, 2024.

Akizungumzia mafunzo hayo, Balozi wa Muungano wa Comoro na Mkuu wa Kikosi cha Wanadiplomasia, Dk Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih, amepongeza mpango huo huku akiutaja kama mwarobaini wa mgawanyiko wa kidijitali barani Afrika.

“Programu hii ni ya wakati unaofaa na muhimu. Ni hatua ya kupongezwa kuelekea kuziba mgawanyiko wa kidijitali barani Afrika,”amesema Dk Fakih

Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey (mwenye tai nyekundu katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi kutoka Afrika katika programu maalum ya Akili Bandia katika Diplomasia iliyoandaliwa na Ubalozi wa India.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mwanakhamis Adam Ameir, amesema Serikali inalenga kuiweka Kampasi ya IIT Madras Zanzibar kuwa kitovu cha elimu barani Afrika.

“Tunawaalika mabalozi kuhimiza uandikishaji wa wanafunzi kutoka nchi zenu. Taasisi hii ni muhimu katika dira yetu ya kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha ubora katika teknolojia,” amesema Mwanakhamis.

Naye, Balozi wa India nchini, Bishwadip Dey, amesisitiza umuhimu wa tukio hilo akisema. "AI ni mustakabali wa diplomasia. Inawezesha uelewa wa kina na kukuza ufanyaji maamuzi bora katika mahusiano ya kimataifa,” amebainisha.

Taasisi hiyo, iliyofunguliwa Oktoba 2023, inatoa programu katika akili ya bandia, sayansi ya data, na miundo ya bahari. Kulingana na Mkurugenzi wake, Prof Preeti Aghalayam, chuo hicho kimeundwa kukuza talanta katika nyanja zinazochipukia.