Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu vijana kukwepa kutumia kondomu

Muktasari:

  • Februari 14 ni siku ya Kimataifa ya Kondomu! Ikiadhimishwa na Siku ya Wapendanao, ni fursa ya kufanya kampeni za elimu, huduma za upimaji na usambazaji wa bidhaa hizo za afya.

Dar es Salaam. Wakati Serikali ya Tanzania ikihamasisha jamii kutumia kondomu, kama mojawapo ya njia za kujikinga na maradhi yakiwamo ya zinaa, imebainika vijana wengi hawana mwamko wa kutumia kinga.

Kukosa elimu, kutojua umuhimu wake, uhaba wa upatikanaji na matumizi ipasavyo ni miongoni mwa changamoto zilizoonekana, kwa vijana wengi walioulizwa sababu ya wao kutotumia kinga.

Wakati Tanzania ikiadhimisha leo Alhamisi, Februari 13, 2025 jijini Dodoma, kimataifa siku hiyo huadhimishwa Februari 14 siku moja na ile ya wapendanao maarufu ‘Valentine Day.’

Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini (NASHCoP), Dk Zeye Nkomela amesema maadhimisho hayo yatafanyika mkoani Dodoma.

Amesema tafiti zinaonesha kupungua kwa matumizi ya kondomu katika mikoa mbalimbali, na hivyo kuongeza hatari ya maambukizi mapya ya VVU na magonjwa ya ngono kwa makundi mbalimbali.

"Bado kuna dhana potofu na unyanyapaa kuhusu matumizi ya kondomu na hivyo baadhi ya watu wamejikuta wanashiriki katika ngono isiyo salama," amesema Dk Nkomela.

Vijana wataja sababu

Mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, Samson Matata (28) amesema alijaribu mara kadhaa kutumia kinga lakini alishindwa kutokana na kukosa elimu sahihi.

“Situmii kabisa, nikivaa tu basi mambo yanaharibika nashindwa kuendelea, kuna nyakati inabana, nasikia unaniumiza kwenye misuli...,” amesema Matata.

Fidelis Mwakyanjala (19) mkazi wa Tunduma, Mkoa wa Songwe amesema hawezi kutumia kinga, licha ya kutokuwa na elimu amesema hakuwahi kupata elimu hiyo mahali popote.

“Nafahamu  kwamba zina kinga maambukizi ya VVU lakini binafsi siwezi kutumia kwani hazina ladha yoyote,” amesema Mwakyanjala.

Mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam, Shadrack Riziki (24) amesema vijana wengi hawatumii kondomu kutokana na utofauti wa mitazamo.

“ Nikitumia ni kama kunakuwa na usumbufu sana,pia gharama nyingine kununua kinga, ndiyo maana wengi wanatumia za msaada, asilimia kubwa vijana inakuwa changamoto,” amesema Riziki.

Kutokana na tabia ya kutotumia kinga, binti mmoja wa miaka 22 (jina linahifadhiwa) mkazi wa jijini la Mbeya anasema aliwahi kupata ugonjwa wa zinaa.

“Niliwahi kupata ugonjwa wa zinaa, nikaenda duka la dawa nikashauriwa kwenda hospitali. Nilihofia unyanyapaa nikamuomba anisaidie dawa, alinipa,” amesema hakupona, hivyo alilazimika kwenda hospitali alikotibiwa na kupona kabisa.

Uhaba wa elimu ya afya ya uzazi unatajwa kuchangia matumizi hafifu ya kondomu.

“Mwishoni mwa miaka ya 1990 kulikuwa na filamu zilizoonyeshwa vijijini kuhamasisha matumizi ya kondomu, kwenye redio na televisheni pia kulikuwa na matangazo mbalimbali ambayo sasa hayapo, si rahisi vijana kujua umuhimu wa kinga,” amesema Amina Ally (52) mkazi wa jijini Dodoma.

Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Edwin Frank (40) amesema asilimia 80 ya vijana wa kiume, hutumia kondomu katika ngono ya kwanza na pili, hata wanaofika mara ya nne baadaye huacha wakijipa moyo kwamba wameshawaamini hata bila kupima.

“Anaacha kutumia kinga hata kama hawajapima bado, yeye anaamini ule ukaribu wa siku chache ameshaijua afya ya mpenzi wake, changamoto iko hapo,” amesema.

Edwin ameongeza kuwa vijana wengi wa kiume, hutumia kondomu kwa lengo la kujikinga na virusi vya Ukimwi na si mimba au magonjwa ya zinaa.

Wadau washauri

Kwa upande wake, muelimishaji rika kwa vijana, Godlove Isdory amesema baadhi ya vijana hawatumii kinga na wanapopata magonjwa ya zinaa huishia kwenda kujitibu kwa kununua dawa duka la dawa