Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu vifo vya mapema kwa wanaoishi na VVU

Muktasari:

  • Eneo la Afrika ndio ambalo limeathiriwa zaidi, likichangia theluthi mbili ya watu wote wanaoishi na VVU duniani.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2024 za Shirika la Afya Duniani (WHO), takribani watu milioni 40.8 walikuwa wakiishi na VVU duniani na watu 630,000 walikufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na Ukimwi.

Eneo la Afrika ndio ambalo limeathiriwa zaidi, likichangia theluthi mbili ya watu wote wanaoishi na VVU duniani. Hasa nchi za kusini mwa jangwa la sahara zenye uchumi mdogo.

Mambo yafuatayo ndio yameonekana kusababisha vifo vya mapema kutokana na wagonjwa kuvamiwa kirahisi na magonjwa hatari nyemelezi.

Mosi ni magonjwa ya kuambukiza. Wakati mfumo wa kinga umeathiriwa kiasi cha kuwa chini, inawaweka katika hatari kubwa ya kupata maambukizi nyemelezi ikiwamo uambukizi mkali wa bakteria mwilini.

Pili ni kifua Kikuu (TB), ugonjwa huo wa mfumo wa hewa ni chanzo kikuu cha vifo vingi duniani kote kwa watu wenye VVU na huweza kuwa ni ishara ya mapema sana ya maambukizi ya VVU.

Tatu ni maambukizi hatari ya ubongo ya bakteria na fangasi ambayo yanaweza kusababisha kifo endapo hatua madhubuti za matibabu hazitachukuliwa.

Nne ni nimonia, uwepo wa mambukizi makali ya mapafu  ni chanzo cha kawaida cha vifo vya mapema, hasa kwa wale walio na mfumo dhaifu wa kinga yaani wenye idadi ndogo ya seli nyeupe (CD4).

Tano ni kuchelewa kugundulika na kupata matibabu mapema. Hii inasababisha kushindwa kuanza haraka kwa dawa za kufubaza makali ya VVU ili kudhibiti virusi hatimaye kunyanyua kinga ya mwili.

Mwenye maambukizi na aliyekuwa bado hajagundulika kuwa na VVU, virusi vina muda zaidi wa kudhoofisha mfumo wa kinga vikiwa katika idadi kubwa na kuongeza uwezekano kupata magonjwa nyemelezi.

Sita ni hatua za juu za ugonjwa na idadi ndogo ya CD4 wakati anapopimwa na kugundulika. Hii ina maana kuwa virusi vimeshambulia na kushusha kinga, hivyo kuna hatari ya kupata magonjwa hatari nyemelezi hata kama atakua ameanza matibabu.

Sababu zingine zinazochangia ni pamoja na upungufu wa damu, magonjwa mabaya ikiwamo  saratani, kuyumba kwa afya ya akili, magonjwa ya moyo na figo na uzingatiaji duni wa matibabu, huduma duni za matibabu na ukosefu wa elimu ya Afya.

Ili kuongeza maisha kwa watu wenye VVU, wanapaswa kushikamana na matibabu ili kupunguza makali ya VVU kila mara kama ilivyoshauriwa na kudumisha mtindo mzuri wa maisha.

Ulaji wa lishe bora yenye matunda, mboga mboga na protini zisizo na mafuta mengi inaweza kutoa nishati ambayo mwili unahitaji ili kubaki imara na kupambana na maambukizi.

Mazoezi mepesi mara kwa mara na shughuli za kimwili ni muhimu kwa afya kiujumla na husaidia mwili kubaki imara.

Epuka kuvuta sigara, unywaji pombe kupita kiasi na dawa za kulevya kwani haya yanadhoofisha mfumo wa kinga, kuingilia ufanisi wa dawa na kufupisha umri wa kuishi.

Kuburudika, kupumzka na kulala angalau saa 8-10 kwa usiku mmoja, hii ni muhimu ili mwilI uweza kurekebisha, kujenga na kufanya kazi vizuri. Pia kushughulikia matatizo yote afya ya akili ikiwamo kudhibiti msongo wa mawazo.