Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kitita cha uzazi chaleta tumaini mikoa mitano Tanzania

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Kwa takwimu za wiki, vifo vya watoto ambao hawajazaliwa vilipungua kwa asilimia 16 na asilimia 75 vifo vya uzazi

Dar es Salaam.  Kitita cha uzazi salama (SBBC) kimepunguza vifo vya watoto wachanga katika vituo vya afya 30 na kwenye mikoa mitano nchini kwa asilimia 75.

Mikoa iliyofikia malengo hayo ni Manyara, Shinyanga, Tabora, Geita na Mwanza ambayo mradi huo ulikuwa ukitekelezwa kuanzia mwaka 2021 hadi 2023.

Kupitia kitita hicho cha uzazi kwenye mikoa hiyo,  idadi ya kina mama na watoto waliofikiwa ni 300,000, vifo vya watoto kabla ya kuzaliwa vilipungua kwa asilimia 18 na kupunguzwa vifo vinavyotokea kwa kila saa 24 kwa asilimia 40.

Kwa takwimu za wiki, vifo vya watoto ambao hawajazaliwa vilipungua kwa asilimia 16 na asilimia 75 vifo vya uzazi. 

Mafanikio hayo kupitia kitita cha SBBC ni kutokana na mafunzo ya mara kwa mara wanayopewa watoa huduma wa afya ngazi ya jamii ya namna ya kukabiliana na matatizo ya kina mama wakati na baada ya kujifungua pamoja na kupatiwa vifaa.

Pia, wauguzi waliwezeshwa kushughulikia kesi ngumu zinazohusiana na ujauzito.

Kwa mujibu wa Mtafiti Mkuu wa SBBC, Dk Benjamin Kamala, kitita hicho kilichoanza kutekelezwa tangu 2021 hadi 2023 kililenga  kupunguza vifo vya uzazi na vya watoto wachanga kwa kuwapa watoa huduma wa afya ngazi ya jamii ujuzi wa kukabiliana na changamoto za uzazi katika hali ngumu.

Hivi karibuni, Dk Kamala amesisitiza kuwa, programu ya SBBC imebadili mfumo wa utamaduni wa vituo vya afya nchini kwa watoa huduma kujengewa uzoefu na kuwa washindani ambao wamechangia kupunguza rufaa zisizo za lazima.

 “Hapo awali, rufaa nyingi zilitokana na wakunga kukosa kujiamini katika kutoa huduma, watoa huduma tulionao sasa wamejiandaa kushughulikia changamoto zinazowakabili wajawazito na kuondoa rufaa zisizo za lazima,”amesema Dk Kamala.

Katika hatua nyingine, amesema takwimu zinazozalishwa kupitia vituo vya afya ndizo zinapaswa kutumiwa na watoa huduma za afya kukabiliana na eneo linaloonekana linachangamoto.

Tanzania imepiga hatua kufikia lengo la Maendeleo Endelevu (SDG) 3.1, linalolenga kupunguza vifo vya uzazi kuwa chini ya 70 kwa kila vifo 100,000 vya watoto wanaozaliwa hai ifikapo mwaka 2030.

Hatua hiyo imefikiwa kupitia mipango mbalimbali ya kimkakati ya afya ya kuboresha huduma za uzazi na huduma za watoto wachanga ikiwemo mpango wa SBBC.

Februari mwaka huu, Waziri wa Afya, Jenista Mhagama akiwa katika mkutano wa 74 wa Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini (ECSA – HC) uliofanyika Lilongwe nchini Malawi, alieleza juhudi zilizochukuliwa kukabiliana na vifo vitokanavyo na uzazi nchini, huku akidokeza  vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka 1,744 mwaka 2018 hadi 1,477 mwaka 2022.

Pia, vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 11,524 mwaka 2018 hadi 6,342 mwaka 2022.