Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kahawa inavyosaidia wazee kurudisha nguvu mwilini

Muktasari:

  • Wengi ambao wamefikia ukongwe, huwa na tatizo la misuli yao kuisha nguvu au kulegea, ugonjwa ambao unafahamika kwa kimombo kwa jina la ‘Sarcopenia’.

Unywaji wa kahawa unasaidia katika kuimarisha misuli ya mwili miongoni mwa wanaume wakongwe, wanasayansi wamebaini. 

Wengi ambao wamefikia ukongwe, huwa na tatizo la misuli yao kuisha nguvu au kulegea, ugonjwa ambao unafahamika kwa kimombo kwa jina la ‘Sarcopenia’.

Ugonjwa huo hulemaza uwezo wa mwanaume kuwajibika kwa kaz za kawaida zikiwamo za nyumbani. Hii ni kwa wale wenye miaka 60 au zaidi.

Kati ya mambo ya kawaida ambayo mtu hawezi kufanya akiwa na ugonjwa huo ni kutaabika anapotembea, kushindwa kupanda ngazi, kuanguka mara kwa mara huku misuli ikidhoofika kabisa.

Japo kisababishi kikuu cha maradhi hayo ni uzee, kukosa kufanya mazoezi mara kwa mara, uzani kupita kiasi, kupungua kwa homoni mwilini na kisukari pia huchangia misuli kulegea au kudhoofika kiasi cha mtu kushindwa kufanya kazi.

Hata hivyo, wanasayansi sasa wamebaini kuwa kafeni ambayo ipo kwenye kahawa inasaidia sana katika kujenga misuli imara au kuimarisha ile inayoelekea kudhoofika.

Kafeni inazuia kutanuka kwa seli za mwili na pia hulemaza chembechembe za sumu ndani ya mwili hasa ile inayofifisha utendakazi wa misuli.

“Utafiti huu unaonyesha kuwa unywaji wa kahawa au kafeni unahusishwa na misuli kuwa imara. Unaonyesha kuwa unywaji wa kahawa na kupata kafeni ni mbinu ya kuzuia kupotea au kupungua kwa misuli miongoni mwa wanaume,” unasema utafiti huo uliofanywa nchini China.

Kutokana na utafiti huo, wito umetolewa kuwe na uhamasishaji wa wa kuhakikisha kuwa unywaji wa kahawa na kafeni unapigiwa upatu kusaidia  wazee na walio na watu wenye  misuli hafifu.