Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maji ya madafu na ubora wake kwa mwili wa binadamu

Muktasari:

  • Lakini unaweza kujiuliza kwa nini maji ya madafu yanapendwa sana na baadhi ya watu?

Huenda ulikuwa hujui lakini kwa sasa unapaswa kufahamu kuwa maji ya dafu ni muhimu kwa mwili wa binadamu kwa sababu huimarisha kinga ya mwili.

Lakini unaweza kujiuliza kwa nini maji ya madafu yanapendwa sana na baadhi ya watu?

Jibu ni moja tu licha ya kinywaji hicho kuburudisha na kupunguza hali ya uchovu wa mwili lakini pia kwa wale wenye mning’inio wa pombe (hangover) huwasaidia kuondosha hali hiyo.

Pia, husaidia kuua bacteria wa aina mbalimbali wakiwamo wale wanaosababisha maambukizi kwenye njia ya mkojo yaani UTI.

Wataalamu wa masuala ya lishe wanasema maji ya dafu husaidia pia kupunguza maumivu wakati wa kupata haja ndogo (mkojo).

Pamoja na faida hizo, maji haya huongeza virutubisho vya aina tano na vyote huwa na umuhimu ndani ya mwili wa binadamu.

Virutubisho hivyo ni pamoja na madini ya calcium, magnesium, potassium, phosphorous na sodium, ambavyo ni muhimu katika mwili wa binadamu.

Unywaji wa maji ya madafu mara kwa mara husaidia kupunguza tatizo la msukumo mkubwa wa damu mwilini.

Wataalamu wa lishe wanashauri maji hayo yanywewe asubuhi kabla ya kutumia chakula chochote au kinywaji.

Kwa watu wanene, matumizi ya dafu huwasaidia kupunguza uzito na kuwaongezea hamu ya kula kutokana na uasilia wake.