Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chips kuku, mayai, baga zinavyochochea maradhi yasiyoambukiza kwa jamii

Muktasari:

  • Haya ndiyo yanayozisumbua nchi zilizo-endelea kwa sasa, lakini katika nchi mas-kini au zinazoendelea kutokana na sababu nyingi, maradhi yanayosumbua zaidi ni yale ya kuambukiza, kama malaria, kifua kikuu, Virusi vya Ukimwi (VVU) na mengineyo.

Unaweza kujiuliza ni kwa namna gani mtindo wa maisha unachangia kusababisha maradhi yasiyoambuki-za.

Haya ndiyo yanayozisumbua nchi zilizo-endelea kwa sasa, lakini katika nchi mas-kini au zinazoendelea kutokana na sababu nyingi, maradhi yanayosumbua zaidi ni yale ya kuambukiza, kama malaria, kifua kikuu, Virusi vya Ukimwi (VVU) na mengineyo.

Lakini hali imebadilika katika miaka ya hivi karibuni katika nchi zinazoendelea iki-wamo Tanzania, maradhi yasiyoambukiza yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa na sasa yanapita yale ya kuambukiza kwa idadi ya watu wanaougua hata kwa vifo vitokana-vyo na maradhi hayo.

Duniani kwa ujumla, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya mwaka jana, maradhi ya moyo na yale yanayohusi-ana na mzunguko wa damu ndiyo yanaoon-goza kwa kusababisha vifo.

Mkuu wa Idara ya Utafiti na Mafunzo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk Pedro Pallangyo anasema ukian-galia orodha ya maradhi matano yanayoon-goza kwa kuua, manne ni yasiyoambukiza.

Akitolea mfano wa maradhi ya moyo, dak-tari huyo anasema yanaweza kugawanywa katika makundi saba, yanayohusiana na msukumo wa damu, moyo kuwa mkubwa au kupanuka, yanayoathiri valvu za moyo na ya watoto ya kuzaliwa na matundu kwenye moyo.

“Kuna watoto wanaozaliwa wakiwa tayari na dosari kwenye moyo, kuna maradhi ya mishipa ya damu kutandwa na mafuta, yapo yanayotokana na maambukizi ya maradhi ya kwenye mwili wa mtu, upande wa kulia wa moyo kupata athari na kusukuma damu nyingi kwenye mapafu ambayo yanawapata zaidi watu wenye historia ya kuvuta sigara kwa muda mrefu au kufanya kazi katika viwanda,” anasema.

Anasema bila kujali ni kundi lipi, kunakuwa na visababishi na sababu hatarishi zinazohusisha maradhi mengine yote yasiyo ya kuambukiza.

Dk Pallangyo anasema kuna sababu zinazoweza kugawanywa katika makundi matano.

Anasema sababu hizo ni pamoja na ile ya kula vyakula vyenye chumvi na mafuta mengi ambayo si salama kwa afya ya moyo na ya damu.

“Jamii zetu zinapika vyakula kwa kuongeza radha ya chumvi, lakini wapo wanaoamua kuongezea mezani chumvi mbichi, hii ni hatari kwa afya na ndiyo hatari zaidi,” anasema.

Hata hivyo, wakati Dk Pallangyo akisema hayo, utafiti unaonyesha ktika miaka ya karibuni, imeonekana ukanda wa Afrika watu wanakula vyakula vyenye mafuta mengi na hasa vile vya kupika kwa haraka maarufu ‘fast foods’.

Inaelezwa kuwa vyakula hivyo vingi hupikwa kwa kutumia mafuta ya wanyama ambayo ndiyo hatari zaidi kwa afya salama.

Lakini Dk Pallangyo anashauri ni vizuri watu wakala vyakula vyenye mafuta kidogo zaidi na ikibidi vyakula visivyo na mafuta na pale wanapotumia mafuta, watumie mafuta ya mimea.

Anaitaja sababu ya pili kuwa ni watu kutumia vilevi.

Namba moja ni sigara ambayo kemikali zake zinaweza kuathiri kiungo chochote kwenye mwili wa binadamu, ikihusisha zaidi moyo na mapafu, hivyo anashauri isitumiwe kabisa.

“Kwenye upande wa pombe, mtu anatumia kiasi gani cha pombe, kwa hiyo kinacholeta shida ni kwamba mtu anakunywa kwa kiasi gani, lakini tunazuia unywaji wa pombe wa kupindukia si kwamba tunazuia pombe mtu asinywe kabisa,” anashauri daktari huyo.

Analitaja kundi linalofuata ni la watu wenye uzito mkubwa uliopindukia ambao ni moja ya sababu hatarishi kwa shinikizo la damu, kisukari na mshtuko wa moyo, bila kujali athari nyingine.

Sababu inayofuata ni kutokuwa na desturi ya kufanya mazoezi, kutokana na maisha kurahisishwa kwa kiasi kikubwa, sasa hivi mtu hutumia muda mfupi sana kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kwa kutumia vyombo vya moto au lifti wenye maghorofa.

Dk Pallangyo ambaye pia ni bingwa wa upasuaji wa maradhi ya moyo anasema, watu kuwa bize kazini na kukosa muda wa kufanya mazoezi, huongeza uwezekano wa kuugua maradhi yasiyoambukiza yanayohusiana na moyo.

Anasema kuna maradhi mengi yenye uhusiano na moyo kwa kuwa viungo mbalimbali vya mwili viko katika mfumo uliounganishwa.

Anafafanua kuwa viungo vyote vinaungana na moyo unategemea mapafu kwa ajili ya oksijeni, figo inategemea ini na moyo, kwa hiyo, kunapokuwa na tatizo katika kiungo kimoja hususan figo, mapafu na ini, vyote vina uhusiano.

Hivyo, kama kimoja kitaathirika kati ya ini na figo au mapafu, mgonjwa anaweza akapata tatizo la moyo pia.

“Damu yote ya kwenye mwili inasukumwa na moyo na inapitia uchujaji kwenye figo, kwa hiyo kukiwa na shida yoyote kwenye figo mwili huanza kujaa maji na hii maana yake moyo unakuwa na kazi kubwa zaidi ya kusukuma maji au kuwa na kiwango kikubwa zaidi ya maji na damu inayotakiwa kukizungusha. Huo ni mfano wa namna kiungo kimoja kinapopata shida kinavyoathiri viungo vingine,” anasema.

Dk Pallangyo anasema mapafu yanahusika zaidi katika kuchuja na kuipa damu oksijeni, ambayo ndiyo gesi inayotumiwa na viumbe hai, kama yataathirika, moyo hupata oksijeni kidogo hali inayosababisha mwili kukosa damu isiyo na virutubisho vinavyohitajika.

Viungo vingine vikiwa na shida vinaleta athari kwenye moyo.

“Kama mtu ni mtumiaji wa sigara, ile sumu yake huenda kujiweka kwenye mishipa ya damu na kuathiri uwezo wa mishipa kusinyaa na kutanuka ili isikume damu kutoka upande mmoja hadi mwingine. Hali hiyo husababisha mishipa hiyo kuziba na kiwango cha damu kinachopita kinakuwa kidogo kuliko kawaida.”

Ulaji wa mafuta na chumvi nyingi

Anasema kwenye ulaji wa mafuta na chumvi nyingi husababishi kuwa na mafuta mengi kuliko inavyotakiwa.

Mafuta hayo mara nyingi huganda kwenye mishipa ya damu na mwisho wa siku inaleta matatizo kwenye moyo.

Je takwimu zinasemaje

Dk Pallangyo anasema kwa Tanzania, takwimu za maradhi yasiyoambukiz zinaongezeka, japokuwa hakuna uhakika kuhusu takwimu za nchi nzima kuanzia ngazi za wilaya na hospitali za rufaa kupaa.

“Mfano JKCI kila siku tunaona wagonjwa wa nje 250 hadi 300, idadi imeongezeka ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita, 2014/2015, tulikuwa tukiwaona wagonjwa 100 hadi 120 kwa siku.

“Ukija kwa wagonjwa wanaolazwa, tuna vitanda 104, lakini kwa sasa kwa wastani tunalaza wagonjwa saba mpaka 10 kwa siku tofauti na mwaka 2015, wagonjwa waliolazwa walikuwa watatu hadi watano kwa siku,” anasema Dk Pallangyo.

Anasema kitakwimu, aina za maradhi wanayofika kutibiwa, wengi ni wale wenye shinikizo la juu la damu.

“Hivi sasa kila wagonjwa wawili tunaowaona, mmoja anashinikizo la juu la damu, hao wanaobaki ndiyo wanaofika wakiuugua maradhi mengine. Pia tumefanya utafiti katika manispaa ya kinondoni na upimaji wa afya katika kituo cha Mnazi Mmoja, kazi hii ilihusisha Mkoa mzima wa Dar es Salaam na tumebaini tatizo ni kubwa,” anasema

Dk Pallangyo anasema JKCI pia walifanya tafiti ambazo zilihusisha mikoa mbali mbali ikiwamo ya Katavi, Arusha, Dodoma, Mwanza, Lindi na Mtwara ambako pia walibaini shinikizo la juu la damu ndilo linaloongoza.

“Kinachosikitisha zaidi, lazima kifanyiwe mkakati ni kuwa shinikizo la damu halina dalili wengi walikuwa hata hawajijui hadi walipokuja kupima, waligunduliwa wakati wa upimaji.”

Anasema wengine wanafika mara ya kwanza wanakuwa tayari wana madhara mbalimbali kwenye figo, kiharusi, uoni hafifu au hawaoni kabisa.

Dk Pallangyo anasisitiza kuwa sababu hizi zote hatarishi ziko chini ya uwezo wa mtu mwenyewe.

Anaweza kuepuka mardahi haya kwa kuhakikisha anashiriki kikamilifu kufanya mazoezi, kuepukana na unywaji pombe kupita kiasi na kuacha kabisa kuvuta sigara zote pamoja na kupanga mlo wenye lishe bora sambamba na kuepuka matumizi ya chumvi na mafuta mengi.

Anasema suala la kupunguza uzito na kuhakikisha uwiano mzuri wa uzito na urefu vyote vipo ndani ya uwezo wa mtu.

“Nawaasa watu wabadilike wajiwekee jukumu la kufanya vipimo vya afya mara kwa mara hata mara moja kwa mwaka, ni vizuri kujua kiwango cha presha, mafuta, kujua urefu na uzito na uwiano wake kama ni mzuri au mbaya, itakusaidia kujua mapema kabla mambo hayajaanza kwenda kombo.”